Pata taarifa kuu
KENYA-ICC-RUTO-SAN'G

Kenyatta: Hatuwezi kuwa ICC kwa pamoja mimi na naibu wangu, ni kinyume na katiba

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesisitiza kuwa haitawezekana yeye na naibu wake William Ruto kuhudhuria kwa pamoja kwenye mahakama ya ICC kujibu mashtaka yanayowakabili kwakuwa katiba ya nchi hairuhusu.

Naibu rais wa Kenya, William Ruto
Naibu rais wa Kenya, William Ruto Reuters
Matangazo ya kibiashara

Rais Kenyatta ametoa kauli hiyo hapo jana na kudai kuwa kamwe haitatokea yeye na naibu wake Ruto wahudhurie kwa pamoja vikazo vya kesi mjini The Hague kwakuwa kufanya hivyo ni kuisaliti nchi na kutendo hicho hakikubaliki.

Kauli hiyo ambayo ni ya kwanza kwa rais Kenyatta kuitoa toka jopo la mawakili wake washindwe kurejesha kesi hizo nchini Kenya ama Tanzania, alitoa kauli hoyo ka jazba akisisitiza kuwa yeye ndiye rais wa Kenya na kwamba haiwezekani wote wawili wakawa mjini The Hague.

Kauli ya rais Kenyatta imekosolewa pakubwa na wataalamu wa masuala ya sheria wakidai kuwa inalenga kutaka kukwepa mkono wa sheria kwa kuwa jinsi kesi itakavyokuwa ikiendeshwa kuna wakati huenda wote wawili yeye na naibu wake wakalazimika kuwepo mjini The Hague.

Kauli ya Kenyatta inakuja wakati huu ambapo naibu wa rais William Ruto na mwandishi wa habari Joshua Arap San'g wakiwa wamewasili mjini The hague tayari kuanza kusikiliza kesi yao ambayo itaanza kuunguruma siku ya Jumanne.

Mwandishi wa habari Arap San'g mwenyewe alishawasili toka siku ya Jumapili huku naibu wa rais William Ruto akitarajiwa kuwasili hii leo mjini The Hague na kupokelewa na balozi wa Kenya nchini Uholanzi.

Wabunge kadhaa toka muungano wa Jubilee nao wamewasili mjini The Hague kuhudhuria vikao hivyo vinavyoanza hapo kesho, kwenye kesi ambayo inatarajiwa kuchukua mwezi mzima.

Kesi hiyo inaanza wakati huu ambapo wabunge nchini Kenya wamepitisha muswada wa sheria wa kutaka nchi yao kujiondoa kwenye mkataba wa Roma unaoitambua mahakama ya uhalifu wa kivita ya ICCm hatua ambayo imezua mjadala mkubwa nchini Kenya.

Ruto anatuhumiwa na mahakama ya ICC kwa kuhusika kwake na vurugu za uchaguzi wa mwaka 2007-2008 vurugu ambazo watu zaidi ya elfu moja (1000) walipoteza maisha na wengine zaidi ya elfu sitini wakikosa makazi.

Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa kesi za Kenya ni moja kati ya kesi ngumu zaidi kuwahi kushughulikiwa na mahakama ya ICC kwakuwa mashahidi wengi muhimu kwenye kesi hiyo wamejiondoa huku baadhi ya mashtaka yakiondolewa na jopo la majaji hali ambayo wataalamu wa sheria wanahoji utayari wa ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa ICC.

Hata hivyo licha ya pigo ambalo mwendesha mashtaka mpya wa mahakama hiyo Mgambia Fatou Bensouda kukabiliwa nazo ameahidi kuendelea na kesi hizo na kwamba ana ushahidi wa kutosha kudhibitisha mashtaka dhidi ya viongozi hao wawili.

Mahakama ya ICC imekuwa ikikosolewa na viongozi wa bara la Afrika kuwa inaendeshwa kisiasa kwakuwa kesi nyingi zinawakabili viongozi wa Afrika, jambo ambalo mahakama hiyo imekanusha.

Hivi karibuni mataifa ya Afrika yalipiga kura na kupitisha mchakato wa mataifa hayo kuanza kujiondoa kwenye mkataba wa Roma unaotambua mahakama ya ICC hatua ambayo ilitokana na shinikizo la rais wa Uganda Yoweri Museveni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.