Pata taarifa kuu
SOMALIA

Rais wa Somalia akanusha wanajeshi wake kuhusika na vitendo vya ubakaji dhidi ya wanawake

Rais wa Somalia ameibuka na kukanusha vikali tuhuma zilitolewa na Shirika la Kimataifa la Kutetea haki za Binadamu la Human Right Watch kuwa askari wake wamekuwa wakitekeleza vitendo vya unyanyasaji dhidi ya wanawake kwenye kambi za wakimbizi nchini humo. 

Rais wa Somalia, Mahmoud Sheikh Mohamed
Rais wa Somalia, Mahmoud Sheikh Mohamed REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Rais Hassan Sheikh Mohamud, amesema kuwa amesikitishwa na ripoti hiyo na kwamba haamini kuwa askari wake wanaweza kutekeleza vitendo vya ubakaji dhidi ya wanawake hasa kwenye kambi za wakimbizi nchini humo ingawa amekiri kufanyia uchunguzi tuhuma hizo.

Siku ya Jumanne Shirika la Human Right Wtach lilitoa taarifa inayowataja askari wa Somalia pamoja na makundi mengine ya usalama kutekeleza vitendo vya ubakaji dhidi ya wanawake ambao wamekuwa wakiomba hifadhi za dharura kwenye makambi yaliyoko nchini humo.

Rais Hassan Sheikh Mohamud amesema kuwa Serikali yake toka imeingia madarakani imekuwa mstari wa mbele uhubiri suala la kuheshimiwa kwa haki za binadamu hasa kwa wanajeshi wake ambao wameanza kushika doria kwenye maeneo mengi ya nchi.

Kiongozi huyo ameongeza kuwa kipaumbele kikubwa kwenye Serikali yake ni kuhakikisha kuwa watu wote waliotajwa kuhusika na vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Katika hatua nyigine nchi ya Sierra Leone inajiandaa kutuma kikosi cha wanajeshi wake 850 kwenda nchini Somalia ikiwa ni kutekeleza mpango wa Umoja wa Afrika kwa nchi wanachama kuchangia wanajeshi nchini Somalia kupambana na wapiganaji wa Al-Shabab.

Kikosi hicho cha wanajeshi kitakuwa chini ya mwavuli wa majeshi ya Umoja wa Afrika AMISOM ambapo rais wa Sierra Leone, Ernest Koroma amewataka wanajeshi hao kuwa wakakamavu katika kuisaidia nchi ya Somalia kuwa na amani ya kudumu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.