Pata taarifa kuu
CYPRUS-EU-ECB-IMF

Benki nchini Cyprus kuendelea kufungwa hadi siku ya Alhamisi

Benki nchini Cyprus zitaendelea kufungwa kwa siku ya pili mfululizo ambapo zinatarajiwa kufunguliwa tena siku ya Alhamisi ikiwa ni siku moja tu toka nchi hiyo ifikie makubaliano na Umoja wa Ulaya EU na shirika la fedha duniani IMF na kupatiwa mkopo wa euro bilioni 10.

Benki kuu ya Nchini Cyprus
Benki kuu ya Nchini Cyprus REUTERS/Bogdan Cristel
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Cyprus, Nicos Anastasiades ametetea uamuzi wa nchi yake kuchukua hatua kali kama hiyo ili kuinusuru nchi hoyo kutumbukia kwenye mdororo wa kiuchumi huku akikiri kuwa wananchi wengi wataathirika na mpango huo.

Akiwahutubiwa wananchi mara baada ya kufikiwa kwa makubaliano kati yake na wakopeshaji toka Umoja wa Ulaya, rais Anastasiades amesema kuwa haina budi kwa nchi hiyo kuchukua hatua kali za kubana matumizi kuinusuru nchi hiyo na mdororo wa kiuchumi.

Kwenye makubaliano hayo yaliyofikiwa siku ya jumapili jioni, ymeshuhudia kufilisiwa kwa benki ya pili kwa ukubwa nchini humo ambapo watu waliokuwa na akiba iliyozidi euro laki moja fedha zao zilitaifishwa na serikali huku walionusurika ni wale waliokuwa na chini ya kiwango hicho.

Akitangaza uamuzi wa kuendelea kuzifunga benki nchini humo, waziri wa fedha wa Cyprus, Michael Sarris amesema amezingatia ushauri uliotolewa na benki kuu ya nchi hiyo kuhakikisha kwanza kunakuwepo mfumo madhubuti utakaohakiki mzunguko wa fedha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.