Pata taarifa kuu
DAVOS-USWIS

Viongozi wa dunia na wadau wa uchumi wanakutana mjini Davos, Uswis kujadili hali ya uchumi wa dunia

Wanasiasa, wafanyabiashara, wasomi na viongozi wa mbalimbali wa dunia wameanza kuwasili mjini Davos Uswis kuhudhuria mkutano wa kimataifa wa uchumi ambao unatarajiwa kujadili hali ya uchumi wa dunia kwasasa. 

Mario Draghi, rais wa Benki ya Umoja wa Ulaya kwenye moja ya mikutano ya WEF iliyofanyiak Davos mwaka jana
Mario Draghi, rais wa Benki ya Umoja wa Ulaya kwenye moja ya mikutano ya WEF iliyofanyiak Davos mwaka jana REUTERS/Christian Hartmann
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya marais toka nchi 45 duniani pamoja na washauri wa uchumi zaidi ya elfu 2500 wanakutana mjini Davos kwenye mkutano wa siku tano utakaojadili hatma ya uchumi wa dunia na kutafuta suluhu ya kujenga imani kwa wananchi wao kuhusu kufufua uchumi wake.

Mbali na viongozi wa dunia, wafanyabiashara na wasomi, pia mamia ya waandishi wa habari toka nchi mbalimbali duniani wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo muhimu wa uchumi unaowashirikisha wadau toka taasisi mbalimbali.

Mkutano huo unafanyika wakati mkutano wa mwaka jana uligubikwa na mjadala kuhusu sarafu ya Euro na mtikisiko wa kiuchumi kwenye nchi ya Ugiriki ambao ulikuwa unatishia uchumi wa dunia.

Akifungua mkutano huo mwanzilishi wa WEF Klaus Schwab amewataka washiriki wa mkutano huo kutazama namna mpya ya kuimarisha uchumi wa Ulaya ambao unaendelea kuwa shakani pamoja na ule wa nchi zinazoendelea hasa bara la Afrika ambako uwekezaji kwenye sekta za uchumi umeongezeka.

Wachambuzi wa masuala ya uchumi wanaona kuwa mkutano wa mwaka huu huenda ukawa na mtazamo chanya kuhusu kuimarisha uchumi wa dunia ingawa bado wanaona kuna changamoto ambazo viongozi wa dunia ni lazima wasimame kidete kunusuru uchumi wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.