Pata taarifa kuu
ALGERIA

Waziri mkuu wa Algeria asema ni raia wa kigeni 37 tu ndio waliouawa kwenye tukio la utekaji nyara

Serikali ya Algeria imetangaza kuwa ni raia wa kigeni 37 ndio waliouawa kwenye tukio la utekaji nyara kwenye kituo kimoja cha gesi kaskazini mwa nchi hiyo ambapo watu zaidi ya 80 walipoteza maisha. 

Wanajeshi wa Algeria wakilinda doria kwenye eneo la kituo cha gesi ambako utekaji nyara ulifanyika juma lililopita
Wanajeshi wa Algeria wakilinda doria kwenye eneo la kituo cha gesi ambako utekaji nyara ulifanyika juma lililopita Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na waziri mkuu wa Algeria, Abdelmalek Sellal amethibitisha kuuawa kwa raia hao wakigeni akisema kuwa wengi walikutwa wameuawa baada ya kupigwa risasi na watekaji nyara wakiislamu.

Waziri mkuu huyo ameongeza kuwa wengi wa waliouawa walikuwa wamepigwa risasi kichwani huku wengine viungo vyao vikitenganishwa na kukatwa na mapanga.

Mwishoni mwa juma hili kikosi maalumu cha makomandoo wa Algeria kililazimika kutumia nguvu kuingia kwenye kituo hicho kwa lengo la kuwaokoa mateka hao.

Waziri mkuu Sellal ameongeza kuwa raia mmoja wa Algeria aliuawa huku rais watano wakigeni wakiwa hawajulikani walipo huku kukiwa na taarifa kuwa wametekwa na wapiganaji hao.

Licha ya kuwepo taarifa za kukinzana kuhusu idadi kamili ya watu waliopoteza maisha kwenye operesheni hiyo bado taarifa zinasema kuwa huenda idadi imezidi watu mia moja huku serikali yenyewe ikisema idadi kamili ya wau waliokufa ni 40.

Tukio la utekaji nyara lililotekelezwa nchini humo lililaaniwa vikali na jumuiya ya kimataifa huku mataifa ya magharibi yakitaka maelezo ya kutosha toka kwa Serikali ya Algeria kuhusu namna operesheni hiyo ilivyoendeshwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.