Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN

Shambulio la bomu lajeruhi watu sita mjini Kabul, risasi zarindima

Watu wenye silaha na wale wa kujitoa muhanga wameshambulia kituo kimoja cha polisi mashariki mwa mji mkuu wa Afhganistan Kabul, ambapo kumeripotiwa makabiliano makali ya risasi kati ya wapiganaji hao na polisi wa Afghanistan. 

Askari wa Afghanistan akikimbiwa mjini Kabul kukabiliana na wapiganaji wa Taliban
Askari wa Afghanistan akikimbiwa mjini Kabul kukabiliana na wapiganaji wa Taliban Reuters
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa polisi kwenye mji huo Mohammad Zahir amesema kuwa watu wawili hadi watatu waliokuwa wamevalia vilipuzi walikuwa wanajaribu kuingia kwenye kituo hicho kabla ya kuzuiliwa na polisi ambapo kulifuatiwa na mashambulizi ya risasi.

Moto ulionekana kuwaka kwenye ghorofa ya kwanza ya jengo la Polisi ambapo inadaiwa ulisababishwa na mlipuko ambao ulitokana na roketi ambalo lilirushwa na wapiganaji hao wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Taliban.

Watu walioshuhudia tukio hilo wanasema kuwa mbali na watu hao kujaribu kuingia kwenye jengo hilo mtu aliyekuwa kwenye gari alijitoa muhanga nje kidogo ya jengo hilo ambapo watu sita wameripotiwa kujerihiwa kutokana na mlipuko huo.

Mashambulizi hayo ni mfululizo wa matukio ambayo yamekuwa yakitekelezwa na wafuasi wa Taliban ambao wameapa kufanya hivyo kama ulipizaji kisasi kutokana na kuuawa kwa wapiganaji wake kwenye maeneo ambayo yanakaliwa na vikosi vya kigeni nchini humo.

Ingawa Polisi wanahusisha tukio hilo na wapiganaji wa Taliban kundi hilo bado halijatoa taarifa iwapo ndilo limehusika na mpango huo wa kutaka kulipua kituo cha Deh Mazang.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.