Pata taarifa kuu
MYANMAR-KACHIN

Majeshi ya Myanmar yashambulia kambi za waasi wa Kachin, wenyewe watishia kuendeleza vita

Majeshi ya nchi ya Myanmar yameshambulia ngome za waasi wa Kachin kaskazini mwa nchi hiyo licha ya agizo la rais kutaka kusitishwa kwa mapigano kwenye eneo hilo na kutoa wito waasi hao kushiriki kwenye mazungumzo. 

Waasi wa Jimbo la Kachin nchini Myanmar
Waasi wa Jimbo la Kachin nchini Myanmar AFP/Soe Than WIN
Matangazo ya kibiashara

Mwishoni mwa juma rais Thein Sein alitoa tangazo kutaka kusitishwa kwa mapigano kwenye mji wa La Ja Yang kwenye eneo la Kachin mpakani mwa nchi hiyo na China na kuwataka waasi kurejea kwenye meza ya mazungumzo.

Msemaji wa waasi wa Kachin amesema kuwa kuwa majeshi ya Serikali yalianzisha mapigano tena siku ya Jumamosi kwa kushambulia kambi zake jambo ambalo linakiuka makubaliano ambayo walikuwa wamefikia na serikali.

Jeshi huru la Myanmar limethibitisha kutekeleza mashambulizi hayo na kuongeza kuwa yalitokana na waasi wenyewe kukiuka makubaliano kwa kuendelea kusonga mbele kutaka kuchukua miji zaidi kwenye jimbo la Kachin.

Kusitishwa kwa mapigano yaliyodumu kwa miaka 17 kwenye eneo hilo yalitiwa saini mwaka 2011 lakini mwanzoni mwa mwaka huu kumezuka mapigano mapya kati ya vikosi vya Serikali na waasi wa Kachin.

Jumuiya ya kimataifa imetaka Serikali ya nchi hiyo kuketi meza moja na waasi wa Kachin ili kumaliza tofauti zao ili kunusuru maelfu ya wananchi ambao wanayakimbia makazi yao kuepuka vita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.