Pata taarifa kuu
DOHA-QATAR-CLIMATE

Mkutano kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa waingia siku yake ya mwisho, nchi bado zavutana

Mazungumzo kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa chini ya Umoja wa Mataifa UN yameingia kwenye siku yake ya mwisho hii leo huku kukiwa hakuna matumaini ya nchi wanachama kufikia makubaliano kuhusu kukabiliana na tatizo hilo. 

Moja ya maeneo yaliyokumbwa na ukame ambao umetokana na uharibufu wa mazingira
Moja ya maeneo yaliyokumbwa na ukame ambao umetokana na uharibufu wa mazingira Reuters
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa nchi wanachama wameendelea kuvutana kuhusu iwapo waongeze muda wa mkataba wa Kyoto ama utiwe saini mkataba mwingine ambao utachukua nafasi ya mkataba wa Kyoto.

Mazungumzo hayo yanayofanyika mjini Doha Qatar yanalenga kujaribu kuyashawishi mataifa yaliyoendelea kiviwanda duniani kupunguza matumizi ya hewa ya carbon ambayo imekuwa na athari kwa mazingira.

Mashirika yasiyo ya kiserikali na wawakilishi toka nchi mbalimbali wamekashifu hatua ya viongozi wa mataifa yaliyoendelea kushindwa kukibaliana na kutia saini kukubali kupunguza matumizi ya hewa chafu.

Mataifa ya Marekani, Canada na Uchina yameendelea kutishia kutotekeleza makubaliano ya Tokyo Japan kwa madai kuwa ni lazima na mataifa mengine kama Uingereza na Ujerumani ambayo yameendelea kiviwanda kukubali kupunguza matumizi ya hewa chafu.

Wachambuzi wa masuala ya mazingira wanasema kuwa iwapo mazungumzo ya hii leo yatamalizika bila nchi wanachama kufikia makubaliano itakuwa pigo kwa utunzaji wa mazingira kwakuwa uchafuzi wa mazingira utaendelea na tabaka la hewa kuendelea kuharibika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.