Pata taarifa kuu
MALI-BURKINA FASO

Waasi wa Ansar Dine na MNLA wakutana kwa mara ya kwanza na viongozi wa Serikali ya Mali

Viongozi wa Serikali ya Mali kwa mara ya kwanza wamekutana na viongozi wa kundi la  Ansar Dine na lile la waasi wa Tuareg MNLA kwenye mazungumzo yanayolenga kujaribu kutafuta suluhu ya mgogoro wa kaskazini mwa nchi hiyo.  

Viongozi wa Kundi la Ansar Dine na MNLA ambao wamekutana na viongozi wa Serikali ya Mali
Viongozi wa Kundi la Ansar Dine na MNLA ambao wamekutana na viongozi wa Serikali ya Mali Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo hayo yanayosimamiwa na rais wa Burkina Faso Blaise Compaore yanalenga kuyashawishi makundi hayo kuheshimu mipaka ya nchi pamoja na kukomesha vitendo vya ugaidi nchini humo na kwenye nchi jirani.

Mazunguzmo hayo yanafanyika wakati ambapo tayari Jumuiya ya nchi za kiuchumi za magharibi mwa Afrika ECOWAS ikiwa imeidhinisha kupelekwa kwa vikosi vya kimataifa nchini Mali kukabiliana na waasi hao.

Hii ni mara ya kwanza kwa makundi hayo yanayoshikilia kaskazini mwa Mali kukubali kufanya mazungumzo na Serikali kujaribu kumaliza tofauti zao kabla ya baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa halijaidhinisha rasmi kuanza kwa operesheni za kijeshi nchini humo.

Wakati wa mazungumzo yaliyofanyika mjini Bamako, waasi hao na viongozi wa Serikali walikubaliana kusitisha mapigano, kuheshimu haki za binadamu pamoja na kukomesha vitendo vya ugaidi nchini humo.

Mazungumzo hayo pia yanalenga kuyataka makundi hayo kuheshimu uhuru wa watu kuabudu bila kuwiangilia pamoja na kukomesha sharia za kiislamu ambazo zimekuwa zikitumika kwenye miji ambayo wanaishikilia.

Rais Compaore alikutana kwa nyakati tofauti na viongozi wa makundi ya Ansar Dine na wale wa MNLA ambapo awali alizungumza na viongozi wa Serikali ya Mali.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.