Pata taarifa kuu
DOHA-QATAR-CLIMATE

Ban: Lazima viongozi mkubaliane kuhusu kupunguza matumizi ya hewa chafu kunusuru dunia

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa UN, Ban Ki Moon ametoa wito viongozi wanaojadiliana kuhusu mabadiliko ya tabia nchi na jinsi ya kupunguza matumizi ya gesi chafu kwa mazingira kuondoa tofauti zao ili kupata suluhu.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon akizungumza kwenye mkutano wa mwaka wa Umoja wa Mataifa kuhusu mazingira mjini Doha, Qatar
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon akizungumza kwenye mkutano wa mwaka wa Umoja wa Mataifa kuhusu mazingira mjini Doha, Qatar Reuters
Matangazo ya kibiashara

Ban amesema kuwa ili kuhakikisha dunia inakuwa salama kutokana na matumizi ya gesi chafu ni lazima nchi wanachama zikubaliane na mpango wa kuhakikisha zinapunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya Carbon ili kunusuru tabaka la hewa.

Kiongozi huyo ameongeza kuwa ni lazima zipatikane fedha za haraka kwaajili ya kuhakikisha zoezi hilo linasimamiwa kikamilifu kwa nchi wanachama kukubali kuidhinisha kiasi kadhaa cha fedha kwaajili hiyo.

Mkutano huo ambao unajumuisha wajumbe toka nchi karibu 200 hapo jana walijumuika na mawaziri wa mazingira zaidi ya 100 pamoja na wakuu wa nchi kwaajili ya hatua za mwisho za mjadala kufikia muafaka kuhusu kupunguza matumizi ya Carbon.

Licha mazungumzo ambayo yaliendelea hadi usiku wa manane mjini Doha, Qatar, bado wajumbe wa mkutano huo wameshindwa kukubaliana iwapo waongeze muda wa mkataba wa Kyoto au la.

Mkataba wa Kyoto unazitaka nchi wanachama hasa zile zenye viwanda vingi kupunguza matumizi ya Carbon pamoja na kutoa fedha za kutosha kwa nchi zinazoendelea ili kuzipa uwezo wa kukabiliana na uharibifu wa tabaka la hewa.

Wataalamu wa masuala ya mazingira wanasema kuwa iwapo nchi za Marekani, Canada, China, Urusi na Uingereza hazitakubali kwasasa kupunguza matumizi ya Carbon basi dunia hasa nchi zinazoendelea zinakabiliwa na hatari kubwa ya kukumbwa na hali joto ambayo ni hatari kwa mazingira na viumbe hai.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.