Pata taarifa kuu
DUNIA

Ripoti: Vitendo vya ugaidi vyaendelea kupungua duniani

Utafiti mpya uliotolewa hivi karibuni kuhusu masuala ya ugaidi umeonesha kuwa vitendo hivyo vimepungua kwa kiasi kikubwa toka mwaka 2007 japo kumeripotiwa vifo vingi kutokana na matukio hayo.

Baadhi ya wapiganaji wa makundi ya Kigaidi wanaoongozwa na kundi la Al-Qaeda
Baadhi ya wapiganaji wa makundi ya Kigaidi wanaoongozwa na kundi la Al-Qaeda Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kwenye ripoti iliyotolewa taasisi ya uchumi na amani imesema kuwa vitendo vya kigaidi vilishamiri zaidi kati ya mwaka 2002 na 2007 na kisha kuendelea kupungua kuanzia mwaka 2007 hadi mwaka 2011 licha ya kushuhudiwa vifo vingi.

Ripoti hiyo imesema kuwa robo tatu ya watu ambao walipoteza maisha kwenye matukio ya ugaidi kati ya mwaka 2002 na 2011 yalirekodiwa nchini Iraq ambako kulikuwa na vita na mashambulizi ya kujitoa muhanga.

Ripoti ya taasisi hiyo ililenga nchi zaidi ya 158 ambazo zimekuwa zikishuhudia matukio ya ugaidi katika kipindi cha miaka 10 ikilenga kuonesha mwenendo wa vitendo vya kigaidi ndani ya miaka hiyo mpaka kufikia sasa.

Ripoti hiyo imeenda mbali zaidi na kuonesha kuwa matukio ya ugaidi yaliongezeka zaidi kwenye mwaka 2005 na 2007 na yalichochewa na machafuko yaliyokuwa yakiendelea nchini Iraq.

Nchi za Pakistan, India na Afghanistan zimerekodi kiwango cha matukio hayo kati ya asilimia 12, 11, na 10 kati ya mwaka 2002 na 2009.

Ripoti hiyo imengeza kuwa licha ya matukio ya ugaidi kupungua kwa kaisi kikubwa bado kuna hatari ya vitendo hivyo kuongezeka kutokana na machafuko yanayoshuhudiwa nchini Syria na kule mashariki ya kati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.