Pata taarifa kuu
BORNO-NIGERIA

Wapiganaji wa Boko Haram nchini Nigeria waua watu 10 kwenye jimbo la Borno

Wapiganaji wa kundi la Boko Haram nchini Nigeria wamewaua watu 10 kaskazini mwa nchi hiyo katika kijiji cha Chibok kwenye jimbo la Borno, polisi nchini humo wamethibitisha.

Wapiganaji wa kundi la Boko Haram nchini Nigeria wakiwa na silaha
Wapiganaji wa kundi la Boko Haram nchini Nigeria wakiwa na silaha Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mamlaka nchini humo zimesema kuwa wafuasi wa kundi hilo walivamia nyumba kwenye mji huo na kuichoma moto kabla ya kuwakamata watu wengine na kuwachinja na kisha kutokomea kusikojulikana.

Kundi la Boko Haram limekuwa likitekeleza mashambulizi ya mfululizo kuwalenga waumini wa dini ya kikristo nchini Nigeria na pia wakipinga utolewaji elimu ya magharibi nchini humo.

Ulinzi umeimarishwa kwenye jimbo la Borno ambako kumetekelezwa shambulio ambapo polisi wamekuwa na msako wa nyumba kwa nyumba kuwasaka watu wanaodhaniwa kutekeleza shambulio hilo.

Mamia ya wananchi wa Nigeria wamepoteza maisha toka kuanza kwa mashambulizi ya kundi la Boko Haram mwaka 2009 ambpo limekuwa likifanya hivyo kushinikiza kuwa na mazungumzo na Serikali.

Shirika la kutetea haki za binadamu nchini Nigeria limesema kuwa zaidi ya watu elfu 3 wamepoteza maisha mpaka sasa kutokana na mashambulizi ya kundi hilo mwaka 2010.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.