Pata taarifa kuu
DUBAI-ITU-UN

Nani awe msimamizi wa matumizi ya wavuti kuwa mjadala kwenye mkutano wa mwaka wa ITU mjini Dubai

Mjadala kuhusu nani msimamizi wa matumizi ya wavuti duniani (Internet) unatarajiwa kuzusha mabishano makali wakati wa mkutano wa mwaka wa shirika la Umoja wa Mataifa la mawasiliano ITU unaotarajiwa kufanyika mjini Dubani kwenye nchi ya falme za Kiarabu UAE.

Picha ikionesha mtandao wa kijamii wa Faceboo ambao unatumiwa na mamilioni ya watu duniani
Picha ikionesha mtandao wa kijamii wa Faceboo ambao unatumiwa na mamilioni ya watu duniani Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo utajumuisha nchi wanachama 193 ambapo baadhi ya wajumbe wa mkutano huo wanataka bodi hiyo ya umoja wa Mataifa ipewe mamlaka zaidi ya kusimamia matumizi ya wavuti duniani.

Mpango huo wa kutaka kuipa nguvu zadi ITU unapingwa vikali na nchi ya Marekani na baadhi ya mataifa ya Ulaya ambayo yanaona kufanya hivyo kunalenga kunyima uhuru wa matumizi ya wavuti kwa wananchi wake.

Hatua ya kutaka bodi hiyo kupewa rungu la kusimamia matumizi ya wavuti inakuja kufuatia hatari inayoendelea kujitokeza kuhusu matumizi ya wavuti ambapo kumekuwa na wizi wa taarifa za siri toka kwa baadhi ya mataifa yaliyoendelea.

Wamiliki wa mitandao ya kijamii pia wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo ambpo nao wamekuwa na maoni tofauti iwapo ITU itapewa mamlaka makubwa zaidi ya kusimamia mitandao ya kijamii na taarifa ambazo zimekuwa zikichapishwa.

Mkutano huo wa siku kumi na mbili unatarajiwa pia kuangalia namna ya kuimarisha usalama kupitia wavuti na jinsi ambavyo nchi zilizoendelea na zinazoendelea zinaweza kushirikiana katika kudhibiti wizi wa njia ya mtandao.

Wajumbe wengine wa mkutano huo wanahofu kuwa iwapo ITU itatoa mamlaka kwa baadhi ya nchi kuwa na uwezo wa kuchunguza taarifa za wavuti,basi taifa la Marekani huenda likawa na uwigo mpana zaidi wa kufanya hivyo na kutishia uhuru wa matumizi ya mitandao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.