Pata taarifa kuu
PAKISTAN

Makabiliano katika kambi ya kijeshi nchini Pakistan yasababisha vifo vya watu 9

Kundi la watu lililokuwa limejihami kwa silaha limevamia kambi ya jeshi la angaa nchini Pakistan na kusababisha kuuawa kwa watu tisa.

Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi makali yameshuhudiwa usiku wa kuamkia siku ya Alhamisi kwa saa kadhaa baada ya kundi hilo kuvamia kambi ya Minhas karibu na mji Mkuu Islamabad na kusababisha kuuliwa kwa wapiganaji wanane na mwanajeshi mmoja.

Kabla ya kuingia katika kambi hiyo, kundi hilo la wapiganaji lilianza kurusha makombora katika kambi hiyo ya kijeshi kabla ya maafisa wa kijeshi kukusanyika na kuanza kukabiliana nao.

Hakuna kundi la kigaidi ambalo limekiri kutekeleza mashambulizi hayo lakini imekuwa ikishukiwa kuwa kundi la Taliban limekuwa likilenga kutekeleza mashambulizi dhidi ya kambi za kijeshi nchini humo hasa ile ya Minhas ambayo ndio kubwa zaidi na ina zana nyingi za kivita.

Maafisa wa serikali ya Pakistan wamekanusha ripoti kuwa kambi hiyo inahifadhi silaha za nuclear.

Majeshi ya Kimataifa yakiongozwa na yale ya kutoka Marekani yamekuwa katika mstari wa mbele kutafuta makundi ya kigaidi kama vile Taliban, katika mashambulizi ambayo Islamabad imekuwa ikiilamu Marekani kwa kuwashambulia wanajeshi wake kimakosa.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.