Pata taarifa kuu
SYRIA

Urusi yasema inamuunga mkono Koffi Annan kuhusu mzozo wa Syria huku mapigano yakiendelea mjini Damascus

Mapigano kati ya wanajeshi wa serikali na wapiganaji wa upinzani yameendelea kushudiwa katika mji wa Damascus kwa siku ya tatu leo.

Matangazo ya kibiashara

Wanaharakati wa haki za binadamu wanasema majeshi ya Syria yanatumia silaha nzito ikiwemo ndege za kivita kuwashambulia wapiganaji hao wa upinzani.

Wakati makabiliano hayo yakiendelea, msuluhishi wa kimataifa kuhusu mzozo huo Koffi Annan amefanya mazungumzo na rais wa Urusi Vladimir Putin kuhusu namna ya kumaliza mzozo huo.

Vladimir amemwambia Annan kuwa Urusi itafanya kila liwezekanalo kufanikisha mpango wake wa kuleta amani nchini Syria.

Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon yuko mjini Beijing China kujaribu kuishawishi Beijing kubadilsiha msimamo wake kuhusu machufko ya Syria.

Urusi na Uchina zimeendelea kushikilia msimamo wao kutounga mkono azimio lolote dhidi ya rais Bashar Al Assad na badala yake kusema suluhu la Syria liko mikononi mwa raia wenyewe wa taifa hilo.

Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wanatarajiwa kupigia kura azimio la kumwekea vikwazo rais wa Syria Bashar Al Assad.

Azimio hilo linatarajiwa kupigiwa kura Jumatano hii, lakini tayari Urusi imesema kuwa itatumia kura yake ya veto kuzuia kupitishwa kwa azimio lolote dhidi ya rais Assad.

Aidha, baraza hilo linatarajiwa kujadili hatima ya waangalizi wa kijeshi nchini Syria ambao wanamaliza muda wao siku ya Ijumaa.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.