Pata taarifa kuu
AFGANISTAN

Mashambulizi ya bomu yatikisa Afganistan

Zaidi ya watu 40 wameuawa nchini Afganistan baada ya kutokea kwa mashambulizi kadhaa ya bomu ya  kujitoa mhanga.

Matangazo ya kibiashara

Shambulizi la kwanza limesababisha kuuawa kwa watu 23 na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa Kusini mwa nchi hiyo karibu na makao makuu ya majeshi ya NATO katika mkoa wa Kandahar.

Mapema leo asubuhi watu wengine 15 wameuawa baada ya majeshi ya NATO kutekeleza shambulizi la angaa lilikuwa linawalenga wanamgambo wa Taliban Kusini mwa mji wa Kabul.

Naibu kiongozi wa mkoa wa Kabul Rais Khan Sadeq Abdulrahimzai amesema miongoni mwa wale waliouawa katika shambulizi hilo ni watoto na wanawake.

Uhusiano kati ya Afganistan na majeshi ya NATO umedorora katika siku za hivi karibuni kutokana na majeshi hayo kushutumiwa kuvamia makaazi ya raia na kusabaisha mauji ya watu wasiokuwa na hatia.

Rais Hamid Karzai ameagiza uchunguzi kufanywa ili kubaini ikiwa waliouawa walikuwa ni raia wasiokuwa na hatia.

Kwa muda wa miaka mitano iliyopita, idadi ya raia wa Afganistan ambao wameuawa kutokana na mashambulizi ya NATO imefikia 3,021.

Marekani ambayo ina wanajeshi wengi nchini Afagnistan inasema itayaondoa majeshi yake nchini humo kufikia mwisho wa mwaka wa 2014.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.