Pata taarifa kuu
Ufaransa

Polisi nchini Ufaransa wazingira nyumba ya mshukiwa aliyetekeleza mauji katika shule ya Kiyahudi

Polisi mjini Toulouse Kusini mwa Ufaransa wanazingira nyumba inayoaminiwa kuwa na mshukiwa aliyetekeleza mauji katika shule ya Kiyahudi mapema juma hili na kusababisha mauji ya watu wanne wakiwemo watoto watatu.

Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa usalama wanasema mama wa mshukiwa huyo amefika katika shule hiyo na anashauriana na maafisa wa polisi kuhusu kukamatwa kwa mwanawe.

Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa Claude Gueant anasema oparesheni ya kumkamata mshukiwa huyo anayetuhumiwa kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la al-Qaeda .

Polisi wawili wamejeruhiwa katika oparesheni hiyo wakati wa ufwatuliaji wa risasi katika oparesheni hiyo.

Tayari miili ya watoto watatu na mwalimu wao,imewasili nchini Israel Jumatano asubuhi tayari kwa mazishi mjini Jerusalem.

Waziri wa nchi wa mambo ya nje wa Ufaransa Alain Juppe amewasili pamoja na miili hiyo pamoja na zaidi ya jamaa wa karibu zaidi ya hamsini.

Hata hivyo,rais Sarkzoy amewahakikishia viongozi wa Kiyahudi nchini Ufaransa kuwa serikali yake inafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa tukio lingine kama hilo halitokei tena na kuongeza kuwa usalama umeimarishwa katika shule zote za kidini nchini humo.

Walioshudia kisa hicho wanasema mtu aliyetekeza mauji hayo awasili katika shule hiyo akiwa na bastola mbili akiwa juu ya pikipiki na kuanza kufwatua risasi kiholela.

Wiki iliyopita,wanajeshi watatu wa Ufaransa waliuawa Kusini mwa nchi hiyo baada ya kupigwa risasi na watu wasiofahamika.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.