Pata taarifa kuu
Marekani-Ulaya

IMF, yafanya uteuzi wa kwanza baada ya kumpata kiongozi mpya

Shirika la fedha duniani, IMF imemteua mchumi nkutoka nchini China, Zhu Min kutumikia nafasi ya naibu mkurugenzi mkuu hatua inayoipa china fursa ya kutambulika mchango wake mkubwa katika uchumi wa dunia.

Christine Lagarde Mkuu wa IMF akiongea na vyombo vya habari kwenye makao makuu ya shirika hilo
Christine Lagarde Mkuu wa IMF akiongea na vyombo vya habari kwenye makao makuu ya shirika hilo REUTERS / Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Zhu, amewahi kutumikia nafasi ya naibu gavana wa Benki kuu ya china na kwa miaka sita alikuwa akihudumu katika benki ya dunia.

Aidha shirika hilo limemteua msaidizi wa ikulu ya marekani, David Lipton kurithi nafasi ya naibu mkurugenzi mkuu msaidizi aliyokuwa akiitumikia, naibu mkurugenzi mkuu wa kwanza, John lipsky.

Lipton aliwahi kuwa mshauri wa Barack Obama katika maswala ya uchumi wa kimataifa. Huu ni uchaguzi wa kwanza wa mkuu wa shirika hilo, Christine lagarde.

IMF inatekeleza mpango wake wa kunyanyua nchi zinazokuwa kiuchumi kwa kuzileta karibu, hasa china, india, Brazil, Urusi, na Afrika kusini.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.