Pata taarifa kuu
UGANDA

Serikali ya Uganda yawaondoa zaidi ya wafanyakazi hewa elfu 5

Serikali ya Uganda imewaondoa zaidi ya wafanyakazi hewa elfu 5 na 500 kutoka kwenye orodha ya watu wanaolipwa mshahara, wakati huu mapambano dhidi ya wafanyakazi hewa na udanganyifu yakiendelea kwenye ofisi za uma.

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, ambaye ameagiza kufutwa kazi na kuondolewa kwenye orodha ya malipo ya Serikali wafanyakazi wasio halali
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, ambaye ameagiza kufutwa kazi na kuondolewa kwenye orodha ya malipo ya Serikali wafanyakazi wasio halali REUTERS/James Akena
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni, aliahidi kukabiliana na vitendo vya Rushwa baada ya kuapishwa kwa muhula wa 5 mwezi Mei mwaka huu, huku taifa lake lilikosolewa pakubwa na nchi wafadhili kwa kukithiri kwa Rushwa.

Waziri wa huduma za uma, Muruli Mukasa, amesema kuwa wanakabidhi orodha ya wafanyakazi hewa kwa Polisi pamoja na mkaguzi mkuu wa Serikali kwaajili ya uchunguzi zaidi na ikiwezekana kufunguliwa mashtaka.

Waziri Mukasa amesema kuwa, kati ya wafanyakazi laki tatu na elfu 8 walioajiriwa Serikalini, wamefanikiwa kuwaondoa wafanyakazi zaidi ya elfu 5 kwenye orodha ya mishahara.

Serikali imesema itatumia mfumo wa kielektroniki kubaini wafanyakazi halali walioajiriwa na Serikali kama ilivyoagizwa na Rais Museveni.

Shirika la kimataifa la Transparency International, limeiorodhesha nchi ya Uganda katika nafasi ya 138 kati ya nchi 168 duniani ambazo zimekithiri kwa vitendo vya Rushwa kwa takwimu za mwaka jana, huku asilimia 80 ya raia wa Uganda wameripotiwa kutoa na kuokea Rushwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.