Pata taarifa kuu
SOKA

Michuano ya kombe la Chalenji yaingia siku ya pili, Burundi yainyuka Somalia 2-0

Michuano ya kombe la Chalenji imeingia siku ya pili huku mechi mbili zikichezwa hii leo kwenye dimba la Machakos jijini Nairobi Kenya ambapo katika mechi ya kwanza baina ya Burundi na Somalia, timu ya Burundi imeibuka na ushindi wa magoli 2-0

Baadhi ya mashabiki wa soka nchini Kenya
Baadhi ya mashabiki wa soka nchini Kenya Ikiwa katika nafasi ya 204 katika orodha ya FIFA iliyotolewa leo
Matangazo ya kibiashara

Katika mechi hiyo ya kundi B, Burundi kupitia kwa washambuliaji wake Christopher Nduwarugira and Abdul Razak imeweza kuilambisha mchanga Somalia Ocean Stars kwa kufunga jumla ya magoli mawili, kila goli likifungwa katika kipindi cha kwanza na cha pili.

Ikiwa katika nafasi ya 204 katika orodha ya FIFA iliyotolewa leo Alhamisi Novemba 28, 2013), Somalia imeonesha mchezo wa hali ya juu dhidi ya Burundi,ambayo inashika nafasi ya 112.

Kwa matokeo hayo sasa Burundi inaongoza kundi hilo huku kwa alama 3, ikifuatiwa na Tanzania yenye alama 1, Zambia timu alikwa ikifuatia ikiwa na alama 1 baada ya kutoka sare ya goli 1-1.

Hapo kesho Ijumaa timu ya Uganda itashuka dimbani kumenyana na Rwanda  kwenye uwanja wa Machakos mtanange ambao unatarajia kuvuta hisia za wengi.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.