Pata taarifa kuu

Wakaazi wa Bujumbura wanakabiliwa na uhaba wa mafuta

Nairobi – Kwa majuma kadhaa sasa, imekuwa vigumu kabisa kwa raia kupata mafuta katika jiji la Bujumbura nchini Burundi, wateja wakilalamika kuzunguka usiku kucha na kila siku kutafuta vituo vyenye mafuta bila mafanikio.

Wakaazi wa Bujumbura wamekuwa wakikabiliwa na uhaba wa mafuta kwa muda sasa
Wakaazi wa Bujumbura wamekuwa wakikabiliwa na uhaba wa mafuta kwa muda sasa Reuters/ Bernadett Szazbo
Matangazo ya kibiashara

Inaelekea miaka miwili sasa tangu kuibuka kwa uhaba wa mafuta nchini Burundi. Viongozi wa nchi hiyo kwa sasa hawatowi tena matumaini ya kupatikana kwa jawabu la swala hili baada ya hatua kadhaa zilizochukuliwa hapo awali kugonga mwamba.

Wadau mbalimbali wametoa wito kwa serikali kuketi kwenye meza ya mazungumzo na wafanyabiashara ya bidhaa hiyo muhimu kutafuta suluhu ya tatizo hilo.

Mara kadhaa rais wa nchi hiyo Evariste Ndayishimiye amesikika akisema kulivalia njuga swala hilo, muda unakwenda hakuna mafaanikio, na hivi majuzi msemaji wake Guillaine Gatoni amesema swala hilo lipo mbioni kupatiwa jawabu, huku wafanyabiashara wa bidhaa hiyo wakinyooshewa kidole cha lawama kuhusika katika tatizo hili.

Hata hivyo wananchi ambao ndio wakwanza kutaabika na sakata hili wameonekana kukata matumaini baada ya kuali kadhaa za viongozi wa serikali pamoja na hatua zilizochukuliwa ambazo hata hivyo hazikuzaa matunda.

Mashirika ya kiraia yamejitokeza hadharani na kuitaka serikali kuketi kwenye meza ya mazungumzo na wahusika wa swala hili kumaliza tatizo na kuwataka viongozi wawajali wananchi zaidi ambao ndio wanaotaabika, kutokana na kwamba viongozi wao hawakosi mafuta.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.