Pata taarifa kuu

DRC: Kamanda mpya wa vikosi vya EAC akabidhiwa majukumu

NAIROBI – Kamanda mpya wa Kikosi cha Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACRF) Meja Jenerali Alphaxard Muthuri Kiugu kutoka Kenya, amekabidhiwa ofisi na mtangulizi wake Meja Jenerali Jeff Nyagah, hapo jana siku chache kupita tangu ajiuzulu.

Meja Jenerali Aphaxard Muthuri Kiugu, kamanda mpya wa vikosi vya EAC nchini DRC
Meja Jenerali Aphaxard Muthuri Kiugu, kamanda mpya wa vikosi vya EAC nchini DRC © EACRF DRC
Matangazo ya kibiashara

Kuanza kazi kwa kamanda huyu mpya kumekuja baada ya kuruhusiwa na serikali ya Kinshasa, ambapo ataanza kutekeleza awamu ya pili ya majukumu ya vikosi hivyo ambayo viliongezewa muda hadi mwezi Juni.

Hata hivyo anaanza kazi katika mazingira yenye utata, hasa baada ya kauli ya hivi karibuni ya rais wa DRC, Felix Tshisekedi, ambaye alivituhumu vikosi hivyo kushindwa kutekeleza majukumu yake ikiwemo kukabiliana na makundi yenye silaha.

Mwezi uliopita Meja jenerali Jeff Nyagha alilazimika kuachia nafasi yake kutokana na shinikizo kutoka Kinshasa, ambapo akadai hata alitishiwa usalama wake, lakini wiki hii utawala wa Nairoibi, uliihakikishia Serikali ya DRC kuisaidia nchi hiyo kuyamaliza makundi ya waasi.

Mbali na kuwa jenerali Kiungu anachukua madaraka katika kipindi chenye utata, ataongoza hata hivyo bila kujua ikiwa vikosi vyake vitaongezewa muda wakati huu jumuiya ya SADC nayo ikitarajiwa kutuma wanajeshi wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.