Pata taarifa kuu

Burundi: Waziri mkuu wa zamani Alain Bunyoni anatafutwa na polisi

NAIROBI – Mamlaka nchini Burundi zimeanzisha msako dhidi ya waziri mkuu wa zamani Alain-Guillaume Bunyoni, miezi saba tangu afutwe kazi.

Waziri mkuu wa zamani wa Burundi Alain-Guillaume Bunyoni
Waziri mkuu wa zamani wa Burundi Alain-Guillaume Bunyoni AFP - TCHANDROU NITANGA
Matangazo ya kibiashara

Bunyoni, ambaye kwa wakati mmoja alikuwa mkuu wa polisi na waziri wa usalama, alifutwa kazi septemba mwaka jana, katika hatua ya mabadiliko ya kwanza makubwa tangu rais Evariste Ndayishimiye kuchukuwa madaraka 2020.

Inaripotiwa kuwa siku ya jumatatu polisi na maafisa wa upelelezi walifanya msako katika makaazi yake matatu, lakini hawakufanikiwa kumpata, waziri wa usalama wa ndani Martin Niteretse akisema bado wanamtafuta Bunyoni.

Afisa mmoja wa juu wa jeshi ameiambia AFP kwamba, wamemkamata afisa mmoja wa polisi ambaye anadaiwa kumtaarifu Bunyoni kuhusu oparesheni ya kumsaka, hali iliomfanya kukimbia kabla ya maafisa wa polisi kufika.

Bunyoni, mtu mwenye ushawishi katika chama tawala cha CNDD-FDD na ambaye aliteuliwa waziri mkuu 2020 alifutwa kazi  siku chache baada ya rais Ndayishimiye kuonya kuhusu mpango wa mapinduzi dhidi yake.

Ndayishimiye alichukua mamlaka mnamo Juni 2020 baada ya mtangulizi wake Pierre Nkurunziza kufariki kutokana na kile mamlaka ya Burundi ilisema ni changamoto za kupumua  huku kukiwa na uvumi ulioenea kuwa aliaga dunia kutokana na Covid-19.

Amesifiwa na jumuiya ya kimataifa kwa kuaanza kuirejesha Burundi katika ulingo wa kimataifa ya kutengwa chini ya utawala wa Nkurunziza. Lakini ameshindwa kuboresha rekodi mbaya ya haki za binadamu na nchi yenye watu milioni 12 inasalia kuwa miongoni mwa nchi maskini zaidi duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.