Pata taarifa kuu

Burundi yatakiwa kuwaachia huru watetezi watano wa haki za binadamu

Mashirika yasiyo ya kiserikali ya haki za binadamu siku ya Jumanne yameizitaka mamlaka nchini Burundi kuwaachilia 'mara moja' watetezi watano wa haki za binadamu waliokamatwa kwa madai ya uasi na kuhatarisha usalama wa taifa. Mashirika hayo yametaka mamalaka ya Burundi kuacha "kutishia" mashirika ya kiraia.

Ofisi ya shirika la Haki za Binadamu la Ligue ITEKA, Bujumbura, Burundi.
Ofisi ya shirika la Haki za Binadamu la Ligue ITEKA, Bujumbura, Burundi. © RFI/Sonia Rolley
Matangazo ya kibiashara

Wanaharakati hao walikamatwa na idara ya ujasusi mnamo Februari 14 wanne kati yao walikuwa kwenye uwanja wa ndege wakijianda kupanda ndege kuelekea Uganda kutoka mji mkuu wa kiuchumi wa Bujumbura, na baadaye kushtakiwa kwa mashtaka haya.

"Mamlaka ya Burundi inapaswa kuwaachilia mara moja na bila masharti watetezi watano wa haki za binadamu waliokamatwa kiholela" na "kufuta mashtaka yasiyo na msingi dhidi yao", shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Amnesty International, Initiative for Human Rights in Burundi na Human Rights Watch yameandika katika taarifa.

Kukamatwa huku na kufunguliwa mashtaka "kunashuhudia kuzorota" kwa hali ya "mashirika ya kiraia yanayojitegemea nchini Burundi", amesisitiza Clémentine de Montjoye, mtafiti katika wa shirika la kimataifa la HRW katika ukanda wa Afrika.

Miongoni mwa wanaharakati wanne waliokamatwa katika uwanja wa ndege ni Sonia Ndikumasabo, kiongozi wa Chama cha Wanasheria Wanawake nchini Burundi na naibu mwenyekiti wa zamani wa Tume Huru ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu. Mfungwa wa tano, Prosper Runyange, mwanachama wa shirika linalotetea Amani na Kukuza Haki za Binadamu (APDH), alikamatwa Ngozi, kaskazini mwa Burundi.

Shutuma hizo "zinatokana tu na uhusiano wao na shirika la kimataifa la kigeni na ufadhili waliopokea kutoka kwa shirika hilo", yanabainisha mashirika hayo yasiyo ya kiserikali, bila kutoa maelezo zaidi. Mnamo mwezi Februari, Waziri mwenye dhamana ya Usalama, Martin Niterese, alisema "kuna uwezekano mkubwa kwamba kuna hatari ya kufadhili ugaidi kupitia fedha hizi".

Tangu aingie madarakani mwaka wa 2020, Rais wa Burundi, Évariste Ndayishimiye, ametofautiana kati ya dalili za uwazi wa utawala, ambao unasalia chini ya ushawishi wa "majenerali" wenye nguvu na udhibiti thabiti wa mamlaka unaoonyeshwa na ukiukwaji wa haki za binadamu ambao unashtumiwa na mashirika yasiyo ya kiserikali. Alimrithi Pierre Nkurunziza, aliyefariki mwaka 2020, ambaye alitawala nchi hiyo kwa mkono wa chuma tangu mwaka 2005.

Burundi, ambayo haina bahari katika eneo la Maziwa Makuu, ndiyo nchi maskini zaidi duniani kwa pato kwa kila mtu kulingana na Benki ya Dunia, ambayo inabaini kuwa 75% ya wakazi wake milioni 12 wanaishi chini ya mstari wa umaskini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.