Pata taarifa kuu
Burundi - Haki

Burundi : Human Right Watch latuhumu utawala wa rais Everiste Ndayishimiye

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Human Right Watch, limesema maafisa wa usalama nchini Burundi wametekeleza dhuluma dhidi ya raia wa Burundi ,wanaoshukiwa kuegemea upande wa upinzani, au kushirikiana na makundi ya watu wenye silaha.

Évariste Ndayishimiye, rais wa Burundi
Évariste Ndayishimiye, rais wa Burundi Tchandrou NITANGA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti yake mpya, Human Right Watch imewahusisha polisi, idara ya ujasusi na vijana wanaogemea chama tawala  kuwashumbulia raia na idara za serikali.

Human Right Watch limesema mamlaka nchini Burundi hajaonyesha nia yoyote ya kuendesha uchuguzi huru, ili kuwachukulia hatua wanaohusishwa na vitendo hivyo vya ukiukaji wa haki za binadamu.

Mtafiti mkuu wa HRW kanda ya Africa, Clémentine de Montjoye, ameutaka utawala wa rais Everiste Ndayishimiye, kuwachukulia hatua za kisheria, maafisa wa usalama wanaohusishwa  na vitendo hivyo vya dhuluma, badala ya kuwalenga wapinzani wake.

Montjoye akisema raia wa Burundi wataacha kuishi na uoga serikali itakapowajibisha wanaohusika na vitendo hivyo.

HRW imesema ripoti yake imegemea ushahidi wa raia 30 wa Burundi, wakiwemo wafuasi wa vyama vya upinzani na watetezi wa haki za binadamu, kati ya Oktoba  2021 hadi April 2022.

Mashirika ya kiraia pia, yamekiri kutazama kanda za video ambazo polisi na wanajeshi walikiri kuhusiaka na mauwaji ya raia.

HRW kadhalika imekosoa Umoja wa Ulaya, Marekani na mataifa mengine kuonyesha nia ya kuboresha  uhusiano na Burundi, licha ya ushihidi uliopo wa mamlaka nchini humo kuendelea kukiuka haki za binadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.