Pata taarifa kuu
KENYA-POMBE-AFYA

Kenya: Madhara ya kiafya yanayotokana na pombe ya mbangara

Nchini Kenya ,katika mwendelezo wa ripoti zetu kuhusu pombe ya inayofahamika kama  Mbagara, inayotengenezwa katika kaunti ya Taita Taveta ,Pwani ya nchi hiyo, Mwandishi  wa  RFI Kiswahili Carol Korir anaangazia athari ya pombe hiyo .

Wauguzi wa hospitali ya rufaa ya Moi mjini Voi,  Maureen Kirighi ,Lennox Ngonyo( Katikat)  na Eddah Kirombo mwanasaijolojia, 12. 8. 2021
Wauguzi wa hospitali ya rufaa ya Moi mjini Voi, Maureen Kirighi ,Lennox Ngonyo( Katikat) na Eddah Kirombo mwanasaijolojia, 12. 8. 2021 © Carol Korir
Matangazo ya kibiashara

Pombe ya Mbangara imekuwa ni utambulisho wa kaunt ya Taita Taveta tangu zamani.

Mzee Njumwa Mwandawa ,mkaazi wa kijiji cha Shigharo ,eneo la Wundanyi ,anasema  Mbangara ilitumika kama kiunganishi katika jamii,lakini amewapoteza ndugu wa karibu kutokana na pombe hii.

“ Ya zamani ilikuwa ya miwa hata babangu alikuwa anakunywa ,lakini vitu vinavyotengenezwa saa hii hata sielewi, mimi nishashuhudia hiyo mbangara, watu wakifariki kufariki,watu watatu mmoja alikuwa ni Mwakavu ,si mtoto wa babangu ndugu yake ,”alisimulia mzee Njumwa.

Joyce Mgaro mama wa watoto watatu naye ana simulizi yake kuhusu mbangara.

“ Huyu wetu anasema sema hakuna kulala,na mimi ni mtu wa kurauka ,sasa tutafanyaje , naye tumwacha akilala ,anaweza hata kulala mwezi mmoja haendi popote ,anategemea kipato hicho changu,” alieleza Joyce Mgaro.

Katika shule ya msingi ya Shigharo  Eileen Kilugha,mwalimu mkuu wa shule hiyo anaeleza namna shughuli za elimu zimetatitizika kutokana na pombe hiyo.

“ Nikiwa hapa mwaka wa 2014, watoto walikuwa 450 lakini sasa wamefika 195.Wazazi wa kiume wameacha majukumu yao nyumbani. Vijana wanafika miaka 40 hawana familia ,hawana familia kwa sababu ya ulevi,”alisikitika bi Kilugha.

Katika hospitali ya rufaa  iliyoko Voi ,kaunti hiyo ya Taita Taveta ,kuna kitengo cha kuwasaidia watu wanaotaka kuacha pombe .

Lennox  Ngonyo muuguzi   katika kitengo hicho ,anaeleza namna uraibu wa Mbangara  umekuwa umekuwa kikwazo cha jami ya Dawida  kupanuka.

Pombe ina kiunga ndani yake kinachoitwa Ethanol. Huzuia madini kama zinc kutumika mwilini. Zinc husaidia katika ukuaji  wa mtu na pia katika kutengeneza manii,”alieleza Lenox.

Ni bayana  wagema na wateja wanaofurahia mbangara ,wana hamu sana ya uhalalshwaji wa  Mbangara.

Sehemu ya jamii hata hivyo ikiangalia madhara ,inapendelea kudhibitiwa kwa mbangara , na ndivyo sheria hiyo inayopendekezwa inavyokinzana na hali halisia katika kaunti hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.