Pata taarifa kuu
MALI-UN-NIGER-Shambulio-Usalama

Mali: UN yatoa heshima za mwisho kwa wanajeshi wa Niger waliouawa

Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Mali Minusma imetoa heshima za mwisho kwa wanajeshi wa Niger waliouawa Ijumaa iliyopia kaskazini mwa Mali.

Umoja wa Mataifa watoa heshima za mwisho kwa wanajeshi 9 wa Niger waliouawa kaskazini mwa Mali.
Umoja wa Mataifa watoa heshima za mwisho kwa wanajeshi 9 wa Niger waliouawa kaskazini mwa Mali. AFP Photo/ Habibou Kouyate
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi hao waliuawa katika shambulio lililodaiwa kuendeshwa na kundi la wapiganaji wa kiislam.

Ni shambulio la kwanza lililosababisha maafa makubwa kwa kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Mataifa nchini Mali tangu kikosi hicho kitumwe Julai mwaka 2013.

Naibu Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Hervé Ladsous amehudhuria sherehe za mazishi, ambazo zilijaa hisia.

Miili ya wanajeshi hao tisa waliouawa imekua ikifunikwa bendera ya Umoja wa Mataifa, huku viongozi mbalimbali kutoka Mali, wawakilishi wa kikosi cha wanajeshi wa Ufaransa kinachoendesha operesheni Barkhane.

Naibu Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Hervé Ladsous, amesema ameguswa na tukio hilo, akibaini kwamba wanajeshi hao wa Niger wametimiza idadi ya wanajeshi thelathini wa Umoja wa Mataifa ambao wameuawa tangu kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa mataifa kiwasili nchini Mali.

Miili ya wanajeshi hao imerejeshwa nchini mwao Niger, ili kuendelea na sherehe za mazishi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.