Pata taarifa kuu
Bangui-Sangaris

Baraza la Usalama la UN kuidhinisha kutumwa kwa vikosi 12.000 jijini Bangui

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UN, linataraji kupitisha azimio litalo ruhusu kutumwa kwa wanajeshi elfu 12 wa kulinda amani nchini jamhuri ya Afrika ya kati wakati huu mapigano yenye sura ya kikabila na kidini yakiendelea kushuhudiwa na ambapo wananchi wamekuwa na hofu kuhusu uwezo wa idadi ya vikosi vya kimataifa vilivyopo nchini humo kuzima machafuko.

Majeshi ya Ufaransa katika Operesheni Sangaris
Majeshi ya Ufaransa katika Operesheni Sangaris
Matangazo ya kibiashara

Ufaransa ambayo hivi karibuni ilituma wanajeshi elfu mbili nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, na ambao wawili hapo jana wamejeruhiwa, imewasilisha pendekezo kwenye baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutuma wanajeshi elf 10 na Polisi 1.800 watatowa mafunzo kwa vikosi vya muungano wa Umoja wa Matafa nchini humo Minusca.

Wanajeshi wa kulinda amani ambao wanataraji kutumwa nchini Jamhuri ya Afrika ya kati kuanzia Septemba 15 ijayo wataundwa na wanajeshi elfu sita wa kikosi cha Umoja wa Afrika Misca kilicho tayari nchini humo sanjari na wanajeshi elfu mbili wa Ufaransa katika opersheni Sangaris. Umoja wa Ulaya pia ilioahidi kutuma vikosi vyake, tayari polisi mia nane wapo jijini Bngui kusaidiana na wanajeshi wa Ufaransa .

Licha ya machafuko kwa kiasi kikubwa kuonekana kupungua, bado mauaji ya hapa na pale yenye sura ya kikabila na kidini yanaendelea kushuhudiwa, hali iliompelekea katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon Kutowa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuingilia kwa haraka sana mzozo huo kuepusha kutokea kwa mauaji ya kimbari kama ilivyo kuwa nchini Rwanda miaka 20 iliopita.

Marekani imetangaza msaada wa ziada wa Dola milioni 22 nchini jamhuri ya Afrika ya Kati.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.