Pata taarifa kuu

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon aitolea wito Jumuiya ya Kimataifa kuongeza wanajeshi zaidi nchini jamhuri ya Afrika ya Kati

Jumuiya ya kimataifa imetakiwa kuongeza wanajeshi zaidi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kufuatia kuendelea kushuhudiwa kuzorota kwa hali ya usalama nchini humo na kukithiri kwa mauaji ya ulipizaji kisasi.Juma hili katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa UN, Ban Ki Moon alitoa wito kwa Umoja wa mataifa kuongeza wanajeshi zaidi nchini humo, kauli iliyoungwa mkono na mkuu wa tume ya haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay ambaye naye anataka kudhibitiwa kwa hali ya usalama nchini humo.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon
Matangazo ya kibiashara

Kauli ya viongoizi hawa imejibiwa na Umoja wa Ulaya ambayo tayari imetuma wanajeshi wake zaidi ya elfu 1 kwenda kuungana na wale wa Ufaransa na vikosi vya kulinda amani toka Umoja wa Afrika MISCA ambao wameshindwa kudhibiti hali ya mambo.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon akiwa mjini Brussels Ubelgiji ameeleza kutoridhishwa na hali inayoshuhudiwa nchini humo.

Kwa upande wake, rais wa Ufaransa, Francois Hollande kwenye mazungumzo yake na rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, amemtaka kuhakikisha anakabiliana na changamoto zinazoshuhudiwa nchini mwake ikiwemo kumaliza makundi yote yanayohatarisha usalama nchini humo.

Katika hatua nyingine msemaji wa ofisi wa Tume ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa, Cecile Pouilly ameonya kuhusu kuzorota kwa usalama nchini humo akitolea mfano matukio ya hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.