Pata taarifa kuu
MAREKANI-VATICAN

Barack Obama amekukutana kwa mazunguzo na Papa Francis mjini Vatican

Rais wa Marekani Barack Obama mara baada ya kumaliza ziara yake kwenye makao makuu ya Umoja wa Ulaya EU mjini Brussels, leo amewasili mjini Vatican nchini Italia ambako atakutana kwa mara ya kwanza na kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Papa Francis mjini Vatican.

Rais wa Marekani, Barack Obama na Papa Francis wamekuna kwa mazungumzo kwa muda wa saa moja leo alhamisi mjini Vatican.
Rais wa Marekani, Barack Obama na Papa Francis wamekuna kwa mazungumzo kwa muda wa saa moja leo alhamisi mjini Vatican. REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo kati ya Papa wa kwanza toka Amerika Kusini na rais wa kwanza mweusi wa Marekani yanatarajiwa kujikita kwenye kutafuta suluhu ya kuondoa matabaka yaliyoko kwenye jamii kati ya watu masikini na tajiri.

Rais obama amesema amekuja kumsikiliza Kiongozi wa kanisa katoliki duniani, ambaye ana mawazo yaliyobarikiwa, juu ya kukabiliana dhidi ya umasikini

Hivi karibuni Papa Francis aliwataka viongozi wa dunia akiwemo rais Obama kuhakikisha wanapambana kukomesha matabaka kati ya watu walionacho na wasio nacho na kuongeza kuwa kuacha hali hiyo iendelee kutaendelea kuigawa dunia.

Katika ziara yake nchini Itali, rais Obama anataraji kukutana kwa mazungumzo na waziri mkuu wa Itali Matteo Renzi, na rais Giorgio Napolitano, bila kusahau kulitembelea sehemu ya makumbusho mjini Rome.

Uhusiano kati ya Itali na Marekani ni mzuri, hata kama Roma inaunga mkono Moscow kwa kukuza maslahi yake ya kiuchumi kupitia Ukraine.

Mgogoro katika Mashariki ya Kati, mazingira, na uhamiaje kati ya raia wa Amerika ya kusini na Amerika ya kaskazini vitazungumziwa katika mkutano huo.

Ni kwa mara ya pili Obama anajielekeza Vatican, baada ya kukutana kwa mazungumzo na Benoît XVI jualai mwaka 2009.

Marekani na Vatican wana uhusiano mzuri wa kidiplomasia kwa kipindi cha miaka 30.

Rais Obama huenda akamualika Kiongozi wa Kanisa katika mwezi wa Septemba, wakati kutakua kukifanyika mkutano mkuu wa jamii mbalimbali kutoka Kanisa katoliki mjini Philadelphia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.