Pata taarifa kuu
MISRI- Sheria

Wafuasi 700 wa Mohamed Morsi wanatarajiwa kufikishwa mahakamani

Wafuasi 700 wa rais mwenye msimamo mkali wa kislam, Mohamed Morsi aliye ondolewa madarakani nchini Misri, wanatarajiwa kufikishwa mahakamani leo jumanee, huku wafuasi wengine 529 wa rais huyo wakiwa wamehukumiwa kunyongwa, hukumu ambayo imetajwa na wadadisi kwamba imechukuliwa kisiasa.

Wafuasi 529 wa rais aliye ondolewa madarakani nchini Misri, Mohamed Morsi, hapa ni katika maandamano ya julai 14, wamehukumiwa adhabu ya kifo.
Wafuasi 529 wa rais aliye ondolewa madarakani nchini Misri, Mohamed Morsi, hapa ni katika maandamano ya julai 14, wamehukumiwa adhabu ya kifo. Khaled Kamel - AFP
Matangazo ya kibiashara

Jumuiya ya Kimataifa imesema inatiwa wasiwasi na hukumu hio, ambayo ni ya kwanza kuchukuliwa dhidi ya idadi kubwa ya wafuasi wa Morsi, tangu jeshi lilipomuondoa madarakani rais huyo aliye chaguliwa chini ya misingi ya kidemokrasia julai 3, baada ya baadhi ya wafuasi wake kuuawa na webgine kukamatwa katika maandamano ya kumuunga mkono rais Morsi ambaye ni kutoka chama cha udugu wa kiislamu.

Wafuasi hao wa Morsi wanatuhumiwa kuhusika katika katika machafuko yaliyosababisha kuuawa kwa askari polisi wawili katika jimbo la Minya, na mashambulizi dhidi ya mali ya uma, majengo ya serikali, na ya kibinafsi yaliyotokea ogasti 14, siku ambayo wanajeshi na askari polisi waliwaua kwa risase wafuasi 700 wa Mohamed Morsi wakati wa maandamano ya kumuunga mkono rais huyo mjini Kairo.

Wataalam katika masuala ya sheria wanasema hukumu hio iliyochukuliwa na mahakama ya mwanzo si ya mwisho, kuna haja ya kukata rufaa, na kuna hatari hatua hio ifutwe au irejelewe, kwani mahakama haikuheshimu kanuni na maadili ya sheria na haki ya msingi ya upande wa utetezi.

Hukumu hii ya kifo ni kubwa zaidi kutolewa kwa watu wengi kwa wakati mmoja kwenye historia ya dunia, hatua ambayo wachambuzi wa mambo wanaona kuwa mahakama haikufuata mchakato sahihi wa kufikia kutoa hukumu hiyo.

Huenda uamuzi huo ukabatilishwa na mahakama ya rufaa kwakuwa mawakili wa watuhumiwa hao tayari wamewasilisha pingamizi lao dhidi ya hukumu ya kifo kwa wateja wao wakisisitiza kesi hiyo kuchukua muda mfupi zaidi kuliko kawaida.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.