Pata taarifa kuu
NIGERIA-Usalama

Nigeria inaendelea kukumbwa na visa vya mauaji

Mamia ya wawakilishiwa kutoka makundi mbalimbali ya kikabila, koo na dini wanaounda raia wa Nigeria wanatazamiwa kukutana leo ili kuzungumzia taifa lao kuhusu namna ya kukomesha mauaji ambayo yanaendelea kushuhudiwa nchini humo.

Uharibifu uliyotekelezwa na kundi la Boko haram mwishoni mwa juma liliyopita, nchini Nigeria,
Uharibifu uliyotekelezwa na kundi la Boko haram mwishoni mwa juma liliyopita, nchini Nigeria, RFI
Matangazo ya kibiashara

Takribani watu 100 wameuawa nchini humo mwishoni mwa juma katika mashambulizi matatu kwenye vijiji tofauti , viongozi wa serikali za mitaa wameeleza jana jumapili.
Mbunge wa mji wa Kaduna kwenye bunge la taifa Yakubu Bitiyong, amesema kuwa jumla ya miili mia moja imepatikana kutoka katika vijiji hivyo baada ya watu wenye silaha kuvamia na kufanya mashambulizi Ijumaa na Jumamosi usiku.

Bitiyong pia alisema idadi kubwa ya wakaazi wamejeruhiwa wakati waasi wapatao 40 wakiwa na bunduki na mapanga , walipovamia vijiji vya Angwan Gata, Chenshyi na Angwan Sankwai, na kuwashambulia wakazi wakiwa wamelala na kuchoma moto nyumba zao.

Mbali na watu hao Mia moja kuuawa, watu wengine zaidi ya saba waliripotiwa kuuwawa na wengine wengi kujeruhiwa baada ya ghasia kutokea pale walipokuwa wakihudhuria zoezi la serikali la kuwaajiri watu katika miji kadhaa nchini Humo.

Tangu mwanzoni mwa mwezi wa aprili mwaka 2011, jimbo la Kaduna, ambalo lina raia wengi wa kikristo, linakabiliwa na machafuko ya kijamii.

Machafuko hayo yalianza baada ya kutangazwa ushindi wa rais Goodluck Jonathan,ambaye ni kutoka jamii ya wakisto wa kusini dhidi ya Muhammadu Buhar, ambaye ni kutoka jamii ya waislamu wa kaskazini, katika uchaguzi wa urais.

Machafuko yaliyotokea kabla ya uchaguzi huo yalisababisha watu zaidi ya 400 na maefu ya raia kuyahama makwao, taarfa hiyo ni kulingana na shirika la kimataifa la haki za binadamu Human Right Watch.

Hali ya mvutano kati ya wanasiasa ilisababisha machafuko kati ya makabili na jamii, huku wakulima kutoka jimbo la kaduna wakiwashambuliya waislamu kutoka jamii ya Hausa na Fulani , ambao wanadaiwa kutokua raia wa taifa hilo la Nigeria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.