Pata taarifa kuu
SYRIA-Diplomasia

Wanadini 13 waachiwa huru na waasi wa Syria

Kundi la wanadini lililokuwa limetekwa na waasi wa Syria katika mji wa Maalula mwezi desemba mwaka jana limeachiwa huru mapema leo asubihi hii baada ya majadiliano yaliosimamiwa na Lebanon pamoja na Qatar na kukabidhiwa viongozi wa Syria.Β  Duru kutoka nchini Syria zimearifu kuwa kuachiwa huru kwa wanadini hao kumefanyika baada ya serikali ya Syria kukubali kuwaacha huru wafungwa 150.

Wanadini wawili kati ya 13 walipokua wakiachiwa huru, jumatatu machi 10 mwaka 2014 katika kijiji cha Jdaidet Yabous, nchini Syria.
Wanadini wawili kati ya 13 walipokua wakiachiwa huru, jumatatu machi 10 mwaka 2014 katika kijiji cha Jdaidet Yabous, nchini Syria. LOUAI BESHARA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Takribani wanadini 13 walitekwa nyara na kundi la waasi wa Syria Desemba 3 mwaka jana wakiwa katika kanisa moja mjini Maalula kitongoji kimoja kaskazini mwa jiji la Damascus chenye kikaliwa na wa kristo wengi.

Kundi la Front Al Nosra linalo fungamana na kundi la kigaidi la Alqaeda ndilo lililokuwa linawashikilia wanadini hao katika mji wa Yabroud karibu na mpaka na Lebanon.

Mateka hao wamewasili mapema leo asubuhi katika mji wa Jdaidet Yabous katika mpaka wa Libanon na Syria baada ya kufanya safari ndefu ya saa tisa iliowatowa mjini Yabroud nchini Syria hadi Syria.

Katika hatuwa nyingine, katikabu mkuu wa Jumuiya ya nchi kiarabu Nabil Al Arabi amesema kiti cha baraza la waasi nchini Syria katika jumuiya hiyo kitasailia kuwa wazi kwa muda wote kundi hilo la waasi wa Syria watashindwa kuunda taasisi zake za utawala.

Katika kikao cha mwisho cha Jumuiya ya nchi za kiarabu machi mwaka 2013, wajumbe walikubaliana kuwapa kiti baraza la waasi wa Syria, lakini hadi sasa baraza hilo limeshindwa kuunda taasisi zake kama serikali halali ili kukalia kiti hicho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.