Pata taarifa kuu
SOMALIA-SHAMBULIO

watu sita wapoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa katika shambulio la kuvizia jijini Mogadishu

Watu sita wameripotiwa kupoteza maisha na wengine kadhaa wamejeruhiwa kufuatia shambulio la bomu lililotegwa kwenye gari mjini Mogadishu nchini Somalia, polisi wamethibitisha.

Shambulio la bomu kwenye makao makuu ya UN jijini Somalia
Shambulio la bomu kwenye makao makuu ya UN jijini Somalia
Matangazo ya kibiashara

Polisi mjini Mogadishu wamethibitisha kutokea kwa shambulio hilo na kuongeza kuwa lilitekelezwa kwenye lango kuu la kuingia kwenye uwanja wa ndege wa mjini Mogadishu ambako pia kuna ngome ya vikosi vya majeshi ya kulinda amani ya Umoja wa Afrika AMISOM.

Kwa mujibu wa taarifa za awali za polisi zinasema kuwa, mtu aliyetekeleza shambulio hilo alipaki gari jirani na kituo ukaguzi cha kuingia kwenye uwanja wa ndege wa Mogadishu na wakati akikaribiwa kukaguliwa alijilipua na kusababisha vifo vya watu 6.

Mbali na eneo hilo kuwa ngome ya vikosi vya AMISOM pia ni jirani kabisa na ofisi za ubalozi wa Uingereza nchini Somalia pamoja na ofisi kadhaa za mashirika ya kimataifa ambayo yako nchini humo kukabiliana na wapiganaji wa kundi la Al-Shabab.

Mpaka sasa hakuna kundi lolote lililotangaza kuhusika kwenye shambulio hilo, ingawa kuna kila dalili kuwa huenda wapiganaji wa Al-Shabab wenye uhusiano na mtandao wa Al-Qaeda wakawa wamehusika na shambulio hilo kufuatia mashambulio yao ya hivi karibuni mjini Mogadishu wakilenga vikosi vya kulinda amani na raia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.