Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN -SHERIA

Jeshi la Marekani laendelea kusisitza juu ya hatuwa ya serikali ya Afghanistan kutaka kuwaacha huru wafungwa 88 wanaoshukiwa ugaidi

Msemaji wa wizara ya ulinzi nchini Marekani Steven Warren amesema hatuwa ya kuwaachia huru wafungwa wa jela la Bagram wanatuhumiwa makos aya ugaidi inaweza kurudisha nyuma juhudi za kuifanya Afghanistan kuwa nchi yenye kuheshimu sheria.

rais wa Afghanistan Hamid Karzai
rais wa Afghanistan Hamid Karzai RFI
Matangazo ya kibiashara

Mwezi uliopita rais Hamid Karzai alitangaza kwamba wafungwa 65 kati ya 88 wanaotuhumiwa kutekeleza vitendo vya kigaidi wataachiwa huru baada ya kukosekana kwa ushahidi wa kutosha, wakati vikosi vya Nato na Marekani vikiendelea kusisitiza kwamba watu hao walishiriki kwa njia moja ama nyingine katika mashambulio dhidi ya vikosi vya kimataifa nchini humo.

Tayari wafungwa hao wamepewa kibali cha kuondoka katika jela, na shguhuli za kuachiwa kwa zimepangwa kuanza siku ya alhamisi, hatuwa ambayo Marekani inasema ni uvunjifu wa makubaliano kati yake na Afghanistan. Kanali Warren amesema Marekani imetowa taarifa zinazo thibtisha kwanini wafungwa hao 88 hakuna hata mmoja anaye stahili kuachiwa huru.

Jela hilo la Bagram lililobatizwa Guantanamo ya mashariki ya kati lilikabidhiwa vikosi vya Afghanistan March mwaka 2013 mbele ya rais Hamid Karzai ambaye alifahamisha kuwa ni hatuwa inayoonyesha ishara ya juhudi za Afghanistan kutaka kujitawala.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.