Pata taarifa kuu
UFARANSA-RWANDA-Mauaji ya kimbari

Kesi ya mauaji ya halaiki yaliyotokea Rwanda mwaka 1994 yasikilizwa nchini Ufaransa

Mahakama kuu mjini Paris nchini Ufaransa inatarajia kuskiliza hii leo kwa mara ya kwanza kesi ya mauaji ya kimbari yaliotokea nchini Rwanda mwaka 1994 ikiwa ni miaka ishirini tangu mauwaji hayo yatokee.

Picha ya zamani ya Pascal Simbikangwa
Picha ya zamani ya Pascal Simbikangwa Interpol
Matangazo ya kibiashara

Mtuhumiwa Pascal Simbikangwa mwenye umri wa miaka 54, na aliyekuwa askari wakati wa utawala wa Rais Juvenal habyarimana anatarajiwa kufikishwa kizimbani kujibu mashtaka yanayomkabili ya uhalifu dhidi ya binadamu; tuhuma ambazo amezitupilia mbali.

Pascal Simbikangwa alizaliwa mwaka 1959 kijijini Rambura, katika mkoa wa Gisenyi magharibi mwa Rwanda. Akiwa mshirika wa karibu wa rais Juvénal Habyarimana, Pascal Simbakangwa alishikilia nyadhifa mbalimbali katika ikulu ya Rwanda. Mwaka 1982, Pascal Simbikangwa alijiunga na kikosi cha ulinzi wa rais, baadae katika mwaka wa 1986, Pascal Simbikangwa alijeruhiwa katika ajali ya gari na kumsababishia madhara fulani. katika mwaka uliyofuata aliteuliwa kufanya kazi kwenye idara ya ujasusi katika m akao makuu ya jeshi, kabla ya kuteuliwa mkuu wa idara ya ujasusi ya Rwanda.

Pascal Simbikangwa anatuhumiwa kuhusika katika mauaji ya wapinzani wa utawala wa rais Juvenal Habyarimana. Anashukiwa pia pia kua mwanaharakati wa karibu ya utawala wa rais Habyarimana ambao ulijulikana kwa jina la "Akazu" ikimaanisha 'watu waliyo karibu na familia ya mtawala". Kundi hili lilikua likiunga mkono kusalia madarakani kwa familia ya Juvenal Habyarimana, na kua juu na jamii ya wahutu.

Anashukiwa pia kushiriki kwa kuanzisha kituo cha Radio na Televisheni kiitwacho (RTLM), kituo ambacho kilichochea chuki dhidi ya watu ktika jamii ya watutsi. Kwa mujibu wa Mahakama Ya Mauji ya Kimbari ya Rwanda ICTR, kituo hiki ni moja ya vifaa  viliyochochea mauaji ya kimbari yaliyotokea Rwanda mwaka 1994.

Aidha, Mashirika ya kiraia yanatarajiwa kuwakilisha upande wa walalamikaji kwenye kesi hiyo ambayo itarushwa moja kwa moja kwenye vituo vya televisheni mjini Ufaransa.

Mwenyekiti wa muungano wa mashirika ya kiraia nchini Ufaransa, Alain Gauthier, amesema kesi hio ni muhimu kusikilizwa nchini Ufaransa ili raia wa Ufaransa wajuwe ukweli kwa yale yaliyotokea nchini Rwanda.

“Kesi hii ya Pascal simbikangwa ni muhimu kwetu kwa sababu kwa mara ya kwanza itasikilizwa nchini Ufaransa, tukijuwa kuwa mauwaji hayo yamefanyika nchini Rwanda miaka ishirini iliyopita kwa hiyo ilikuwa jambo muhimu kusikiliza kesi hiyo, na itakuwa fursa kuwaeleza wafaransa ukweli wa mambo katika mauwaji hayo, kutoa hukumu kwa mmoja wa watuhumiwa kwa sababu ni yeye ndiye atakayehukumiwa na sio mauwaji kiujumla”, amesema Alain Gauthier.

Hayo yakitarajiwa, Shirikisho la Kimataifa la Haki za Binadamu la FIDH linaelezea kuridhishwa kwake na kesi hiyo ambayo imesubiriwa kwa siku nyingi.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Kimataifa la Haki za Binadamu la FIDH, Patrick Baudoin ni, amesema kesi hio ni mfano mzuri kwa taifa la Ufaransa, ambalo limeonekana kwa kipindi kirefu kuwapokea wakimbizi wa Rwanda, hasa baadhi ya viongoizi waliyohudumu katika utawala wa hayati rais Juvenala Habyarimana.

“Ni kesi muhimu sana kwa sababu itasikilizwa nchini Ufaransa, na nchi hii ya Ufaransa imekuwa moja kati ya mataifa yanayopinga kuwafungulia mashtaka watuhumiwa wa mauwaji ya kimbari ya Rwanda.

Ufaransa imepokea wakimbizi wengi wa Rwanda na kumekuwepo na hali ya kuwalinda ambayo haikuwawajibisha.

Ufaransa iliunga mkono serikali ya Habyarimana kisisasa na kijeshi, amesema Baudoin.

Wakati huohuo, uongozi wa waasi wa Rwanda waishio mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wa FDLR unathibitisha kuweka silaha chini tangu tarehe 30 mwezi Desemba mwaka uliopita.

Uamuzi huo unafwatia msimamo wa vikosi vya kimataifa vya kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo vya MONUSCO wa kuwasaka na kuwapokonya silaha waasi hao, ikiwa ni kipaumbele cha vikosi hivyo kwa mwaka 2014 na tayari harakati za kujianda kwa operesheni hiyo zinaendelea kuripotiwa.

Waasi hao wameomba viongozi wa nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu kusimamia mchakato wa uwekaji silaha chini na kuwasaidia kuwasiliana na serikali ya Kigali kwa mazungumzo ya amani.

Kaimu mwenyekiti wa waasi wa FDLR, Jenerali Victor Byiringiro, amesema wanasubiri Jumuiya ya Kimataifa kushughulikia madai yao.

“Tutakuwa wazi, maana yangu ni kwamba kuwaomba viongozi wa Afrika kuingilia kati ni kwa sababu wanataka Rwanda iwe na amani na nchi hii ya Congo iwe na amani. Naamini kuwa watatusaidia kutatua tatizo na tutawaonyesha kuwa tulichokisema ni ukweli na tutawakabidhi silaha zetu”, amesema Byiringiro.

Watu yumkini 800,000 kutoka jamii ya watutsi na wahutu wenye msimamo wa wastani waliuwawa,baada ya kifo cha rais Juvenal Habyarimana mwaka 1994.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.