Pata taarifa kuu
UMOJA WA AFRIKA-AU

Nchi za Afrika kuunda kikosi cha dharura kitakacholinda usalama wa maeneo yenye migogoro

Viongozi wa nchi za Afrika wamekubaliana kuendelea kuchukua hatua zaidi kudhibiti machafuko yanayozikumba nchi wanachama sambamba na kuunda kikosi cha dharura kitakachoshughulikia migogoro inayolikumba bara hilo, azimio hilo limefikiwa jana katika siku ya mwisho ya mkutano wa viongozi wa Umoja wa Afrika AU mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.

REUTERS/Tiksa Negeri
Matangazo ya kibiashara

Viongozi walioshiriki mkutano huo wa siku mbili wametaka kuchukuliwa kwa hatua za haraka ili kuikoa nchi ya Sudani Kusini na Jamhuri ya Afrika ya Kati ambazo zinakumbwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.

Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti mpya wa AU ambaye ni Rais wa Mauritania, Mohamed Ould Abdel Aziz amesema nchi wanachama zitatoa wanajeshi watakaounda kikosi hicho.

Mkuu wa Kamisheni ya AU, Nkosazana Dlamini Zuma amethibitisha kuwa tayari mataifa nane yameahidi kutoa wanajeshi wake katika kikosi hicho ambacho mchakato wake ulijadiliwa pia katika mkutano wa mwaka jana wa umoja huo.

Nchi zilizoahidi kutoa wanajeshi wake ni Algeria, Angola, Chad, Ethiopia, Guinea, Mauritania, Afrika Kusini, Tanzania na Uganda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.