Pata taarifa kuu
LEBANON

Mlipuko wa bomu wagharimu maisha ya watu zaidi ya tano akiemo waziri wa zamani wa fedha mjini Beirut

Waziri wazamani wa fedha, akiwa pia balozi wa zamani wa Lebanon nchini Marekani ameuwawa katika shambulio la bomu liliokua limetegwa ndani ya gari. Shambulio hilo limewauwa pia watu zaidi ya tano na wengine zaidi ya sabini kujeruhi. Mohammad Chatah amekua akijielekeza katika mkutano uliyo kua umeandaliwa na muungano wa vyama vya upinzani nchini Lebanon.Kiongozi wa muungano wa vyama vya upinzani nchini Lebanon, Saad Hariri , amelaumu wanamgambo wa Hezbollah mshirika wa Damascus katika shambulio lililomuawa leo ijumaa, mshauri wake wa karibu, Mohammad Chatah.

Matangazo ya kibiashara

"Kwa upande wetu , tunawatuhuma waliyohusika na mauwaji haya, ambao ni hao wanaokwepa vyomba vya kimataifa, wale wanaokataa kuonekana mbele ya mahakama ya kimataifa," amesema Hariri katika taarifa yake akikumbushia tu Mahakama maalum kwa ajili ya Lebanon ( TSL ) kuwajibika kwa kutambua na kuwashitaki wale waliohusika katika kifo cha baba yake , Rafik Hariri.

Wanamgambo wa tano wa kundi hilo la Hezbollah wanasakwa na mahakama hio kwa kuhusika katika kifo cha kiongozi huyo mkuu wa upinzani, lakini Hezbollah inakakataa kuwafikisha mbele ya mahakama. Kesi ya wanamgambo wanne kati ya hao watanu inatazamiwa kuanza kusikilizwa Januari 16 katika kitongoji cha Leidschendam, mjini The Hague.

"Hawa ni wale wanaotaka kuiweka taifa la Lebanon na raia wa Lebanon katka hali ya machafuko," amesema waziri mkuu wa zamani wa Lebanon, akimaanisha kwamba Hezbollah ambao wapiganaji wanamgambo wake wamekua wakipambana dhidi ya waasi nchini Syria, wakishirikiana na jeshi la serikali ya nchi hio.

"Wale ambao wamemuua Mohammad Chatah ndio haohao ambao walimuawa Rafik Hariri, na lengo lao ni kuiteketeza Lebanon”, amesema akisisitiza Hariri.

Saad Hariri, amebaini kwamba mauwaji ya mshauri wake akiwa pia rafiki yake wa karibu, ni kitendo cha ugaidi, ambacho kimeanza sasa kuwalenga.

Tangu mwaka 2005, mfululizo wa mashambulizi yaliwaua wanasiasa tisa , ikiwa ni pamoja na Chattah na waandishi wa habari ambao walikua wakiupinga utawala wa Bashar al- Assad. Maafisa watatu waandamizi wa jeshi na polisi , ambao wawili kati yao walikua karibu na Saad Hariri , waliuwawa pia katika mwaka 2005 na 2012.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.