Pata taarifa kuu
SYRIA-LEBANONI-UINGEREZA

Mwili wa Daktari mwingereza aliyeuawa nchini Syria wakabidhiwa kwa familia yake nchini Lebanon

Mwili wa Daktari mwingereza Abbas Khan aliyefariki dunia akiwa gerezani nchini Syria, umekabidhiwa kwa familia yake na maafisa wa Uingereza nchini Lebanon jana Jumamosi huku familia ikidai kuwa serikali ya Syria imehusika na kifo chake.

Mwili wa daktari mwingereza Abbas Khan  aliyeuawa nchini Syria ukiwasili nchini Lebanon
Mwili wa daktari mwingereza Abbas Khan aliyeuawa nchini Syria ukiwasili nchini Lebanon
Matangazo ya kibiashara

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch pia limeweka shinikizo kwa mamlaka nchini Syria, likiishutumu serikali kwa kusababisha maafa kutokana na mashambulizi ya anga kwenye mji wa Aleppo.

Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) na Shirika la Msalaba Mwekundu la nchini Lebanon wamesindikiza mabaki ya mwili wa Khan kutoka Syria hadi Lebanon kwa msafara wa magari matatu.

Katika juhudi za kidiplomasia , mjumbe wa amani Lakhdar Brahimi amefanya mazungumzo na waziri wa mambo ya kigeni wa Iran, baada ya wasuluhishi kushindwa kukubaliana kuhusu umuhimu wa Tehran kwenye mkutano wa amani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.