Pata taarifa kuu
SYRIA

Iran na Saudi Arabia zaalikwa kushiriki mazungumzo ya amani ya Syria yatakayoanza Januari 22 mwakani

Iran na Saudi Arabia ni miongoni mwa Mataifa zaidi ya 30 yaliyoalikwa kushiriki mkutano wa mazungumzo ya amani kuhusu Syria unayotarajiwa kuanza mwezi Januari mwakani. Mazungumzo hayo yaliyopewa jina la Geneva 2 yanafuatia mkutano wa mwaka 2012 ambao uliokusudia kutafuta suluhu ya mgogoro wa Syria uliodumu kwa takribani miezi 33 na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 120,000.

United Nations/Mark Garten
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo hayo yataanza tarehe 22 mpaka 25 Januari katika jiji la Montreux nchini Uswisi, imebainika kuwa hayatofanyika mjini Geneva kama ilivyoarifiwa hapo awali.

Kwa mujibu wa Mjumbe wa nchi za Kiarabu na Mpatanishi wa mgogoro huo Lakhdar Brahimi, mpaka sasa nchi 32 zimeorodheshwa kushiriki mkutano na huenda ingawa huenda idadi hiyo ikaongezeka kutokana na mahitaji.

Iran na Saudi Arabia ni Mataifa yenye ushawishi mkubwa katika eneo la Mashariki ya Kati, Iran imekuwa ni mshirika mkubwa wa serikali ya Rais wa Syria Bashar al-Assad wakati Saudi Arabia imekuwa ikiupinga utawala huo.

Wanachama watano wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambao ni Marekani, Uingereza, Ufaransa, Urusi na China watashiriki mkutano huo. Wakati Ujerumani na Uingereza ni miongoni mwa Mataifa yaliyoalikwa.

Utawala wa Syria na wapinzani wake wanatarajiwa kutuma wawakilishi katika mkutano huo na watakuwa na mazungumzo ya ndani yatakayoongozwa na Lakhdar Brahimi tarehe 24 ya mwezi Januari.

Serikali ya Rais Bashar al-Assad na wapinzani watatuma wawakilishi tisa kila upande na wote wametakiwa kuwasilisha orodha yake kwa Umoja wa Mataifa UN tarehe 27 mwezi huu.

Uteuzi wa wajumbe huenda ukawa na changamoto hasa kwa upande wa upinzani ambao umekuwa na mgawanyiko huku wengine kusema hawatashiriki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.