Pata taarifa kuu
UFARANSA-JAMUHURI YA AFRIKA YA KATI

Operesheni ya majeshi ya Ufaransa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati yaanza mjini Bangui

Operesheni ya majeshi ya Ufaransa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati imeanza kwa doria kufanyika katika mji mkuu wa Bangui, Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian amesema.

Ufaransa imeagiza majeshi zaidi katika taifa hilo koloni lake la zamani ikiwa ni masaa machache baada ya ghasia za kidini
Ufaransa imeagiza majeshi zaidi katika taifa hilo koloni lake la zamani ikiwa ni masaa machache baada ya ghasia za kidini
Matangazo ya kibiashara

Waziri huyo Le Drian ameiambia Radio France Internationale,kuwa tayari doria imeanza mjini Bangui.

Ufaransa imeagiza majeshi zaidi katika taifa hilo koloni lake la zamani ikiwa ni masaa machache baada ya ghasia za kidini zilizosababisha vifo takribani watu mia moja na ishirini mjini Bangui.

Muda mfupi baada ya Baraza la Usalama kutoa mpango wake wa kuingilia kijeshi, Rais wa Ufaransa Francois Hollande aliamuru takribani askari mia sita kuelekea nchi hiyo ya Afrika, ili kuongeza nguvu iliyokuwepo mjini humo.

Tayari operesheni imepangwa Libreville tangu kuwasili jana na leo ndege zitaanza kusambazwa katika maeneo.

Libreville ni mji mkuu wa jirani Gabon kikosi cha jeshi la Kifaransa kimeundwa na wale askari wapatao mia hamsini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.