Pata taarifa kuu
SYRIA-Shambulizi

Mpiga picha wa kujitegemea auawa na wanamgambo wa Al Qaeda nchini Syria

Waasi wa kundi la Al Qaeda wamemteka nyara na kumwua mpiga picha wa kujitegemea wa Iraq anayefanya kazi Kaskazini mwa Syria , shirika linalosimamia uhuru wa vyombo vya habari limearifu leo Alhamisi.

Waasi wa Al Qaeda nchini Syria
Waasi wa Al Qaeda nchini Syria www.globalresearch.ca
Matangazo ya kibiashara

Unyama huu uliofanywa kwa mpiga picha Yasser Faysal al-Joumaili ni tukio la kwanza kufanywa kwa mwandishi habari mgeni hasa kwenye maeneo ambayo yanasemekana kuwa yamekombolewa nchini Syria amesema kiongozi wa wanahabari wasio na mipaka Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini Soazig Dollet.

Joumaili amekuwa akifanya kazi kama mpigapicha wa kujitegemea kwa chombo cha habari kisichofahamika cha nchini Uhispania katika jimbo lenye mzozo la Allepo nchini Syria kwa karibu siku 10 ameeleza Dollet .

Aidha ameongeza kuwa Joumaili alitekwa nyara na wapiganaji wa jimbo la kiislam la Iraq wakati akiwa njiani kuondoka Syria na kuuawa kwenye mpaka wa Kaskazini Magharibi wa jimbo la Idlib jana Jumatano.

Awali Joumaili alifanya kazi na kituo cha Al -Jazeera English na Reuters,na alikuwa ameoa na watoto watatu.

Miezi ya hivi karibuni kundi la ISIL limeteka nyara makumi ya wanaharakati na watoa habari nchini Syria pamoja na waandishi habari kadhaa wa kigeni.

Kundi hilo lenye mizizi yake kwenye tawi la Al Qaeda la nchini Iraq , limewahi kutuhumiwa kumwua mtangazaji Mohammad Saeed ambaye alikuwa akifanya kazi kwenye kituo cha habari cha Al Arabiya jimboni Aleppo mwezi October.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.