Pata taarifa kuu
Ukraine-Maandamano

Mawaziri wa nchi wanachama wa NATO wakashifu matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji

Mawaziri wa Mambo ya nje kutoka nchi wanachama wa NATO wamekashifu utumizi wa nguvu kupita kiasi unaotumiwa na maafisa wa usalama kupambana waandamanaji wanaotaka kujiuzulu kwa serikali.

Baadhi ya waandamanji walijitokeza katika jiji la Kiev kuonesha gadhabu yao dhidi ya serikali.
Baadhi ya waandamanji walijitokeza katika jiji la Kiev kuonesha gadhabu yao dhidi ya serikali. REUTERS/Vasily Fedosenko
Matangazo ya kibiashara

Mawaziri hao wameitaka serikali ya Ukraine kusikiliza sauti ya wananchi wake na kuacha kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji hao.

Naye Waziri Mkuu Mykola Azarov ameomba msamaha akiwa bungeni kutokana na namna polisi wanavyoendesha oparesheni yao dhidi ya waandamanaji hao ambao wamekuwa wakiandama kwa wiki moja sasa.

Wiki iliyopita, waandamanaji hao waliingia katika barabara za jijini la Kiev na miji mingine kuonesha gadhabu zao dhidi ya serikali kwa kukataa kutia saini mkataba wa ushirikiano na Umoja wa Ulaya.

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani John Kerry ametoa wito kwa upinzani na serikali kuketi katika meza ya mazungumzo na kupata suluhu la kudumu ili kumaliza mzozo huo.

Mswada wa kukosa imani uliowasilishwa bungeni na upinzani kutaka kujiuzulu kwa serikali ulishindwa kufua dafu.

Mapema jumanne bunge la Ukraine lilitupilia mbali jaribio la kushinikiza serikali ya nchi hiyo kujiuzulu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.