Pata taarifa kuu
DRC-M23-UN

Wanamgambo wanao shutumiwa kwa vitendo vya ubakaji na mauaji ya raia nchini DRC wasema wako tayari kuweka silaha chini

Wanamgambo wanaoshutumiwa kwa ubakaji na mauaji ya raia katika eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamesema wako tayari kuweka silaha zao chini, mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa amesema jana Ijumaa, na kulitaka jeshi nchini humo kurejesha utulivu katika maeneo ya jirani. 

Sehemu ya wapiganaji toka makundi ya waasi yanayofanya shughuli zao mashariki mwa DRC
Sehemu ya wapiganaji toka makundi ya waasi yanayofanya shughuli zao mashariki mwa DRC Reuters
Matangazo ya kibiashara

Wanamgambo wa kujilinda wakiongozwa na jenerali Sheka Ntabo Ntaberi anayejulikana kama Sheka Mai Mai limekuwepo nchini humo kwa miaka mitatu sasa, likipambana na majeshi pinzani kwa ajili ya udhibiti wa migodi ya dhahabu.

Mwishoni mwa mwezi Oktoba, Kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini humo, MONUSCO,kiliarifu kwamba takribani raia 34, ikiwa ni pamoja na watoto 20 wenye umri kati ya miezi sita na miaka 17 waliuawa kwa ghasia kubwana na kundi la Sheka Mai Mai katika vijiji vya jimbo la Masisi huko Kivu Kaskazini.

 

 

 

 

 

 

 

Hayo yanajiri wakati huu ambapo kwa mara ya kwanza rais Joseph Kabila  ametembelea mji wa Rutshuru huko Mashariki mwa Congo, Mji ambao awali ulidhibitiwa na kuwa makao makuu pia ngome ya kijeshi ya kundi la waasi la M23.

Rais Kabila amewaahidia wananchi wa Rutshuru amani na usalama wa kudumu baada ya kufanya safari ya urefu wa kilomita mia tisa kwa njia ya gari Mashariki mwa Congo kuonyesha imani yake kuhusu kuimarika kwa usalama katika eneo hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.