Pata taarifa kuu
DRC

Wabunge wa chama cha upinzani cha MLC kinacho ongozwa na Jean Pierre Bemba nchini DRC wasitisha kushiriki vikao vyote vya bunge nchini humo

Wabunge wa chama cha upinzani cha MLC nchini DRCongo kinacho ongozwa na Jean Pierre Bemba Gombo aliyewahi kuwa makamu wa rais na ambaye anashikiliwa na mahakama ya kimataifa ya ICC, Huko The Hague Uholanzi, wameamua kusitisha kushiriki vikao vyote vya Bunge nchini humo. 

Kiongozi wa chama cha MLC nchini DRC Jean Pierre Bemba
Kiongozi wa chama cha MLC nchini DRC Jean Pierre Bemba hirondelle.org
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa msemaji wa chama hicho wabunge hao wanasema wamesikitishwa na hatua ya kukamatwa kwa wanachama wake wanaotuhumiwa kutoa nyaraka za kuihadaa mahakama ya ICC ili kumsafisha Bemba.

Jana Jumatano majaji wamemsikiliza Bemba na kumtaka kujieleza kuhusiana na nyaraka zilizokuwa zimeandaliwa kuihadaa mahakama hiyo, kitu ambacho Jean Pierre Bemba ametetea.

Wabunge wa chama cha MLC wametupilia mbali madai ya mahakama ya ICC kwamba uliandaliwa mtandao wa mashahidi wa uongo wakiwa na nia ya kumsafisha Bemba, Huku mmoja wa waliokamatwa ambaye pia ni mbunge wa kitaifa huko DRC, Fidele Babala akielezea kughadhibishwa na kitendo cha polisi kuvamia nyumbani kwake wakati alipokamatwa.

Wachambuzi wa masuala ya siasa huko DRC wanasema wameshangazwa na kitendo cha kuwakamata wanachama hao wanne wa MLC kwa kuwa kilikuwa ni chama pekee cha upinzani kilichokubali kushiriki mdahalo wa kitaifa uliofanyika mnamo mwezi Septemba iliyopita.

Katika hatua nyingine raisi Joseph Kabila wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, ameendelea na ziara yake Mashariki mwa nchi hiyo, na hii leo Alhamisi atawahutubia wananchi wa Beni na Butembo ambao wanasubiri kwa hamu kujua nini mpango wa serikali kuhusiana na masuala ya usalama katika eneo hilo baada ya kutimuliwa waasi wa kundi la M23.

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.