Pata taarifa kuu
SYRIA

Jeshi la Syria la rejesha udhibiti wa mji wa Deir Attiyeh kwenye himaya yake

Jeshi la Syria limedhibiti tena mji muhimu wa Deir Attiyeh leo Alhamisi , siku chache baada ya kuupoteza, ikijiweka katika nafasi nzuri katika juhudi zake za kuwasambaratisha waasi Kaskazini mwa Damascus.

Wanajeshi wa Syria wakishangilia baada ya kufanikiwa kurejesha mji wa Deir Attiyeh
Wanajeshi wa Syria wakishangilia baada ya kufanikiwa kurejesha mji wa Deir Attiyeh Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kurejesha udhibiti wa mji wa Deir Attiyeh katika barabara kuu ya Damascuss kuelekea Homs kunakuja majuma mawili ya kuwa mikononi mwa mashambulizi ya jeshi katika mkoa wa Qalamoun mkoa muhimu kwa serikali kutokana na ukaribu wake na mji mkuu na waasi kutokana na kwamba unatumika kama ngome ya mwisho iliyo karibu na mpaka na Lebanon.

Pia tukio hili linajiri huku kukiwa na juhudi za kimataifa kufanya mkutano wa amani wa Geneva unaolenga kumaliza mzozo wa miezi 32 nchini Syria.

Wapinzani wanataka mazungumzo yoyote yatakayofanywa yaelekeze katika kipindi cha mpito ambacho serikali ya rais Bashar Al Assad haitahusika kwa namna yoyote.

Hata hivyo askari tiifu kwa rais Assad wameonekana kushinikiza ushindi katika mapambano mengi iwezekanavyo kwa ajili ya kujikweza katika mazungumzo ya mjini Geneva yaliyopangwa kufanyika mnamo Januari 22 mwaka ujao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.