Pata taarifa kuu
IRAN-SYRIA

Iran yasema iko tayari kushiriki mkutano wa Geneva kuhusu Syria bila masharti

Nchi ya Iran ambayo ni mshirika mkubwa wa serikali ya Rais Bashar al Assad imesema iko tayari kushiriki mazungumzo ya amani baina ya Syria na wapinzani wake lakini haitakubali masharti yoyote endapo watalazimishwa kufanya hivyo.

Wanadiplomasia wa mzozo wa Syrian John Kerry, Lakhdar Brahimi and Sergei Lavrov mjini Geneva
Wanadiplomasia wa mzozo wa Syrian John Kerry, Lakhdar Brahimi and Sergei Lavrov mjini Geneva theguardian.com
Matangazo ya kibiashara

Iran ni miongoni mwa mataifa yenye ushawishi mkubwa katika ukanda wa Mashariki ya kati lakini bado haijajulikana iwapo itaalikwa kushiriki mazungumzo au la, mpaka pale itakapotolewa orodha ya waalikwa.

Hayo yanajiri wakati huu Iran ikiwa imeweka makubaliano na jumuiya kimataifa kuhusu mpango wake wa nyuklia inagawaje makubaliano hayo yanaendelea kukosolewa na mataifa mbalimbali pamoja na bunge la Congress la Marekani.

Hali hiyo imemlazimu waziri wa mambo ya kigeni wa marekani John Kerry kutoa somo kwa Congress kuhusu urutubishaji wa uranium na makubaliano yaliyofikiwa baina ya Iran na Jumuiya ya kimataifa.

Mkutano wa amani kuhusu Syria  umetangazwa kufanyika Januari 22 mwaka ujao huku waandaaji wa mkutano huo wakitarajia kwa mara ya kwanza kushuhudia wapinzani na serikali ya rais Bashar Al Assad wakikaa meza moja kujadiliana kuhusu amani ya taifa hilo.
 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.