Pata taarifa kuu
Syria-mkutano

Ufaransa yasema rais Bashar Al Assad na Upinzani hawatashiriki mkutano wa Geneva

Mazungumzo ya amani kuhusu Syria yaliyo cheleweshwa kwa muda mrefu yatafanyika mnamo Januari 22 mwaka ujao huko Geneva Uswis,huku kukiwa na ripoti za kutoshiriki kwa rais wa Syria Bashar Al Assad au makundi ya upinzani yenye msimamo mkali. 

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa Laurent Fabius.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa Laurent Fabius. swahilivilla.blogspot.com
Matangazo ya kibiashara

Hayo yamebainishwa na waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa Laurent Fabius,ambapo ameeleza kuwa lengo la mkutano wa Geneva si kuwa na mazungumzo ya kukutanisha wahusika wa pande zote mbili bali ni kuwa na makubaliano baina ya wawakilishi wa serikali bila uwepo wa rais Assad na wapinzani wenye msimamo wa wastani ili kuunda serikali ya mpito.

Aidha Fabius amekiri kuwa jambo hilo ni gumu ingawa ndio suluhu pekee ambayo inawarurusu wao kwa wakati mmoja kutokuwa na rais Assad pamoja na waasi ambao ni wapinzani katika mkutano huo.

Kauli hii ya Fabius inakuja siku moja baada ya Marekani na Urusi kuweka shinikizo nyuma ya mzungumzo hayo yaliyocheleweshwa kwa muda mrefu yaliyopewa jina la Geneva 2, ambayo Umoja wa Mataifa umesema kuwa hatimaye yatafanyika Januari 22 mwaka ujao.

Msuluhishi wa kimataifa na Jumuiya ya nchi za kiarabu kwenye mgogoro huo Lakhdar Brahimi amesema kuwa bado idadi ya washiriki wa mkutano huo haijaandaliwa kwa ajili ya majadiliano ambayo yatawaleta pamoja serikali ya Syria na upinzani kwenye meza ya mazungumzo kwa mara ya kwanza tangu kuzuka kwa upinzani dhidi ya Assad mwezi Machi mwaka 2011.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.