Pata taarifa kuu
UFARANSA-JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

Ufaransa yathibitisha kupeleka wanajeshi zaidi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

Serikali ya Ufaransa kupitia wizara yake ya ulinzi imethibitisha kuwa imetuma mamia ya wanajeshi wa ziada kwenda kusaidia kuimairisha hali ya usalama nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati.

Waziri wa ulinzi wa Ufaransa Jean Yves Ledrian
Waziri wa ulinzi wa Ufaransa Jean Yves Ledrian deegaan.com
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa ulinzi Jean -Yves Ledrian ameweka wazi kuwa askari hao wa Ufaransa watafanya kazi ya usaidizi kwa kikosi cha askari wa Afrika wanaolinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa kipindi kifupi cha muda wa miezi sita.

Maafisa ya Umoja wa Mataifa wamesema hali ya usalama na ya kibinadamu nchini humo ni ya wasi wasi huku ikionya huenda mauaji ya halaiki yanaweza kuendelea.

Kwa upande wake waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius anasema ni muhimu sana kwa wakati huu kuchukua hatua za dharura ili kuepukana na maafa zaidi,

Mapema  siku ya Jumatatu waziri mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Nicolas Tiangaye baada ya mazungumzo na Laurent Fabius jijini Paris, alisema kuwa waziri Fabius amezungumzia kuongeza askari 800 kwenye kikosi cha askari 410 wa Ufaransa ambao tayari wamo nchini humo kwenye mji mkuu Bangui.

Tiangaye amesema kuwa makosa makubwa ya kivita yamekuwa yakitekelezwa nchini humo ambapo waasi waliompindua madarakani rais Francois Bozize mnamo mwezi Machi na tangu wakati huo serikali ya mpito imepoteza uwezo wa kuongoza watu wapatao milioni 4.5 wa taifa hilo.

Ufaransa ilipendekeza uamuzi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuvipa mamlaka vikosi vya kimataifa kutumia nguvu kumaliza vurugu nchini humo.

Pendekezo hilo ambalo litaweka vikwazo vya kijeshi katika eneo hilo lililoathiriwa na vita, huenda likapitishwa na wajumbe 15 wa baraza la usalama la umoja wa mataifa juma lijalo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.