Pata taarifa kuu
MISRI-MAREKANI

Muslim Brotherhood chaituhumu Marekani kuchangia kupindua utawala wa raisi Morsi.

Chama cha Muslim Brotherhood cha nchini Misri kimetupilia mbali maoni ya waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry kuwatuhumu kuhujumu mapinduzi kwa kile inachoona kuwa Washington ilishiriki kumuondoa madarakani raisi Mohamed Morsi.

Baadhi ya wafuasi wa Chama cha Muslim brotherhood cha nchini Misri wakiwa katika moja ya maandamano
Baadhi ya wafuasi wa Chama cha Muslim brotherhood cha nchini Misri wakiwa katika moja ya maandamano alarabiya.net
Matangazo ya kibiashara

Ghasia zimeikumba Misri tangu jeshi la nchi hiyo lililpompindua madarakani raisi Mohamed Morsi mnamo mwezi Julai kufuatia maandamano ya umma dhidi ya utawala wake uliodumu kwa mwaka mmoja kwa tuhuma za kujilimbikizia madaraka.

Waziri Kerry alitetea uamuzi wa jeshi na Washington ikasema kuwa raisi Morsi alishindwa kukidhi matakwa ya raia,kuwa muwazi na kuzingatia kanuni za kidemokrasia.

Morsi anakuwa kiongozi wa kwanza kuchaguliwa kuwa raisi na kupinduliwa kijeshi kabla ya kuziba nafasi ya Hosni Mubarak ambaye aliondolewa madarakani kwa maandamano ya umma mwaka 2011.

Waziri Kerry siku ya jumatano alisema kuwa Chama cha Muslim Brotherhood ni chama ambacho kimehujumu mapinduzi ya taifa hilo.

Katibu wa Chama cha Muslim Brotherhood Mahmoud Hussein amejibu kauli ya Kerry kuwa Chama cha Brotherhood kilishinda kiti cha raisi na wabunge baada ya kupinduliwa kwa Hosni Mubarak kwa kura zilizosimamiwa kwa uwazi na jeshi.

Aidha Hussein ameituhumu Marekani kushiriki katika kuuondoa utawala wa raisi Morsi madarakani.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.